Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgodi wa Buzwagi kufufuliwa upya
Habari za Siasa

Mgodi wa Buzwagi kufufuliwa upya

Mgodi wa Buzwagi
Spread the love

PAMOJA na mmiliki wa sasa wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, kampuni ya Acacia  Mining, kutangaza kutaka kufunga mgodi wake, serikali ya Tanzania imesema, mgodi huo, uatendelea  kufanya kazi.  Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Acacia iliamua kuufunga mgodi wake wa  Buzwagi, uliyopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga,  baada ya kujiridhisha kuwa utajiri wa madini uliyopo katika eneo hilo, umemalizika.

Taarifa ya mgodi huo kuendelea kutumika, imetolewa leo Jumanne, tarehe 19 Januari 2021 na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa,  Prof. Palamagamba Kabudi, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Madini ya LZ Nickel Limited.

Akizungumza katika halfa hiyo, mbele ya rais John Magufuli, Prof. Kabudi alisema, “faida kubwa ya mradi huu, ni kuanza matumizi mbadala ya miundombinu iliyokuwa inatumika kwenye uendeshwaji wa mgodi wa Buzwagi, ambao unatarajiwa kufungwa hivi karibuni.”

Alisema, muwekezaji huyo mpya, ameomba kwa serikali kuruhusu kutumika kwa miundombinu ya mgodi wa Buzwagi, pindi mgodi huo utakapofungwa.

Aidha, kampuni hiyo imeomba kibali cha kuchenjua masalia ya madini yaliyoko katika mgodi wa Buzwagi, kwa maelezo kuwa teknolojia yake ya kuchenjua masalia hayo kuwa madini, yaweza kufanya kazi hiyo.

Alisema, “…mheshimiwa rais, wawekezaji hawa wameomba mgodi huu utakapofungwa wauchukue ili badala ya kufungwa ufanye kazi nyingine, ili kuuongezea uhai zaidi sababu wanasema yale masalia yaliyoko pale Buzwagi bado yana madini.”

Ameongeza, “…na kwa teknolojia hii mpya, bado watavuna madini haya ambayo sasa ni rundo. Teknolojia ya wale ilikuwa haiwezi kuyachenjua. Hawa wanaweza; sasa masalia yote ya Buzwagi yatarudishwa tena kwenye mitambo na kutoa madini.”

Prof. Kabudi alitoa taarifa hiyo wakati anataja faida za mkataba huo wa uchimbaji madini ya Nickel katika mgodi wa Kabanga mkoani Kagera na ujenzi wa Kiwanda uchakataji madini mkoani Shinyanga.

Ametaja faida nyingine za mradi huo, ni kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini.

“Mradi huu utaongeza ukuaji wa sekta ya madini, kwa kuanzisha na kuendeleza uchimbaji wa madini ya Nickel na madini muambata kama kopa na kobati,” ameeleza.

Prof. Palamaganda Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Prof. Kabudi amesema, mradi huo utasaidia uanzishwaji wa viwanda vinavyotumia masalia ya madini ya metali, kwa ajili ya kutengeza vitu mbalimbali ikiwemo betri za magari.

“Mradi huo, utasaidia kuweka mazingira mapana ya kuanzisha viwanda vinavyotumia mazao ya mwisho ya bidhaa za madini ya metali nchini, mfano sisi wenyewe kukaribisha wawekezaji wa kujenga viwanda vya betri za magari ya umeme na vifaa vya umeme Tanzania,” ameeleza Prof. Kabudi.

MwanaHALISI Online, haikuweza kuwapata wamiliki wa kampuni hiyo, kueleza iwapo watakubali kutoa mitambo yao na malighafi zilizopo katika mgodi huo.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia Mining imekuwa kwenye mahusiano magumu na serikali, tokea mwaka 2017.

Serikali imekuwa ikiituhumu kampuni hiyo kwa kukwepa kodi, udanganyifu na kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kinyume na sheria.

Januari mwaka 2019, ilitozwa faini ya kiasi cha dola za Marekani 130,000, kwa tuhuma za uchafuzi wa mazingira katika mgodi wake wa North Mara.

Acacia imekanusha madai hayo wakidai kila wakifanyacho ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania na mikataba ya ndani na ya kimataifa waliyoafikiana.

Mgogoro kati ya Acaccia na Tanzania uliibuka Machi 2017, baada ya Rais  Magufuli, kutangaza kuzuia makontena ya mchanga wa madini, makinikia; ya kampuni hiyo kusafirishwa nje ya nchi.

Mwaka 2017, serikali ya Tanzania ilidai kuwa inaidai Acaccia dola bilioni 190 ambazo ni kodi ambayo kampuni hiyo ilikwepa kuilipa tokea ilipoanza shughuli zake nchini.

Japo Acacia ilakana madai hayo, kampuni mama ya Barrick Gold Mining Limited,  ilikubali kufanya mazungumzo na serikali na kufikia makubaliano ya kuanza upya “kuaminiana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!