October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meneja wa Diamond akutwa na Corona

Sallam Sharrif, Meneja wa Wasafi Classic

Spread the love

SALLAM Sharif, Meneja wa Msanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekutwa na maambukizi ya virusi aina ya Corona baada ya kufanyiwa vipimo na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Sallam amethibitisha hayo kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram hivi punde na kuishukuru wizara ya Afya kwa msaada walimpatia mpaka hivi sasa na kutaka watu wandelee kuchukua tahadhali.

“Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na corona virus kwa sasa nipo vizuri na afya yangu inaimalika vizuri.” aliandika meneja huyo.

Meneja huyo ambaye hivi karibuni alitembelea nchi mbalimbali barani Ulaya kwenye ziara ya matamasha mbalimbali na msani wake kabla ya kuzuiliwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuamua kurudi nchini.

Mpaka sasa Wizara ya Afya chini ya Waziri Ummy Mwalimu imethibitisha kuwa na wagonjwa sita walipimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar.

error: Content is protected !!