September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa wa corona wafika watano

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

WATU waliokutwa na virusi vya ugonjwa wa corona (COVID -19), nchini Tanzania wamefika tano. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusaini wan a Ummy Mwalimu leo tarehe 19 Machi 2020, wagonjwa hao ni Watanzania waliotoka nje ya mipaka.

“Napenda kutoa taarifa ya mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini, katika masaa 24 yaliyopita baada ya taarifa yangu ya jana.

“Wagonjwa wapya wawili wamethibitika katika jiji la Dar es Salaam kuwa na COVID-19 na hiyo kufanya jumla ya wagonjwa waliothibitika nchini mpaka sasa kufika watano,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza, wagonjwa wote wawili ni wanaume ambapo wote wa umri wa miaka 40.

“Wagonjwa wapya wawili,  mwanaume Mtanzania (40) alisafiri nchi za Uswizi, Denmark na Ufaransa kati ya tarehe 05 – 13 Machi na kurudi nchini tarehe 14 Mchi. Mwingine Mtanzania (40) alikwenda Afrika Kusini kati ya tarehe 14 hadi 16 Machi,” imeeleza taarifa hiyo,” imeeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!