April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Waliokuwa na dereva taxi Arusha, hawajaambukizwa COVID-19’

Spread the love

DAKTARI Janeth Mghamba, Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Ufutiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko katika Wizara ya Afya amesema, watu 27 waliochukuliwa ili kupimwa kama wana maambukizi ya virusi vya corona jijini Arusha, wapo salama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Amesema, watu walioshukuliwa vipimo ni wale waliobainika kuwa na mawasiliana ama kukutana na dereva wa taksi ambaye alimbeba mgonjwa wa kwanza wa corona nchini.

Mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 19 Machi 2020, akiambatana na Dk Faraja Msemwa ambaye ni Mtaalam wa Majanga wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Mghamba amesema sampuli za watu hao baada ya kupimwa walibaini kutoadhiriwa na virusi hivyo.

“Hawa walikuwa karibu na dereva na baada ya kuchukuliwa vipimo, wamebainika hawajaambukizwa,” amesema

Amesema, licha ya taarifa hiyo ya kutoathiriwa na virusi hivyo, wataendelea kufuatiliwa mpaka watakapopimwa kwa mara ya tatu kama ambavyo WHO iliagiza.

error: Content is protected !!