Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe kuzikwa Jumanne ijayo
Habari za Siasa

Membe kuzikwa Jumanne ijayo

Marehemu Bernard Membe enzi za uhai wake
Spread the love

 

JAJI Mustapha Ismail Kambona, msemaji wa familia ya marehemu Bernard Kamilius Membe, aliyeaga dunia mapema leo asubuhi, ametangaza kuwa mazishi ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini, yatafanyika Jumanne ijayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Membe aliyepata kuhudumu kwenye wadhifa wa waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, alifariki dunia, asubuhi ya leo, 12 Mei 2023, katika hospitali ya Kairuki, iliyopo maeneo ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Jaji Mustapha, mwili wa Membe utazikwa kijijini kwao Chiponda, jimboni Mtama, mkoani Lindi, tarehe 16 Mei 2023.

Membe aliyezaliwa 9 Novemba 1953, katika Kijiji cha Rondo, Chiponda, alikuwa mmoja wa mawaziri wandamizi katika serikali ya Kikwete. Alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuwa mrithi wa Kikwete baada ya kuondoka madarakani, Novemba 2015.

Hata hivyo, harakati za Membe na Kikwete mwenyewe, kutaka kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano, ziligonga mwamba.

Pamoja na kwamba jina la Membe lilikuwa miongoni mwa majina matano yaliyofikishwa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa ajili ya kupigiwa kura, lakini hakuweza kupenya.

Alikuwa ni John Pombe Magufuli, aliyetajwa kuwa mshindi wa kura uteuzi. Akiwatupa washindani wake wengine wane – Membe, Balozi Amina Salum Ali, Dk. Asha-Rose Migiro na January Makamba.

Katika kipindi chote cha miaka sita ya utawala wa Rais Magufuli, ni Membe pekee aliyeweza kutoka hadharani kumkosoa kiongozi huyo aliyekuwa anaogopwa nchini Tanzania.

Hivyo basi, wadadisi wa mambo wanasema, “hakuna shaka kuwa kifo chake, kitakuwa pigo kubwa kwa siasa za Tanzania na demokrasia yake, kwa miaka mingi ijayo.”

Katika hatua nyingine, mmoja wa madaktari wa familia ya kiongozi aliyefariki dunia ghafla, Prof. Haroun Ngoyi amesema, mwanasiasa huyo hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya.

Alisema, “Membe alikuwa mzima na mwenye afya iliyoimalika. Hakuwahi kuwa na tatizo sugu kama presha, moyo au sukari. Kilichotokea ni kwamba alipata maambukizi ya ghafla ya mfumo wa mapafu ambayo imesababisha mgando wa damu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!