Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanakijiji Kinyang’erere waepukana na adha ya usafiri
Habari za Siasa

Wanakijiji Kinyang’erere waepukana na adha ya usafiri

Barabara ya kiwango cha rami
Spread the love

 

WANAKIJIJI zaidi ya 4,000 wa Kinyang’erere, Musoma Vijijini mkoani Mara, wameepukana na adha ya usafiri baada ya Serikali kujenga barabara inayowaunganisha katika maeneo yanakopatikana huduma za kijamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Wakizungumza wakati barabara hiyo ya Masinoni-Kinyang’erere, inafunguliwa, baadhi ya wanakijiji wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wake.

Wanakijiji hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Cha Kinyang’erere, Juma Masjilingi, wamesema awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya usafiri kutokana na ukosefu wa barabara.

Walisema kuwa, baadhi ya kina mama wajawazito walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta Huduma ya kujifungua, huku baadhi yao wakijifungulia kichakani Hali iliyokuwa inahatarisha usalama wa maisha Yao.

“Kabla ya kupatikana barabara hii kina mama walikuwa wanatembea kwa mguu kwenda Hospitali kujifungua, wengine walikuwa wanajifungua kichakani kitendo kilichokuwa kinahatarisha usalama wa maisha Yao. Hata wanafunzi nao wakati wa mvua walikuwa wanashindwa kwenda shule sababu kulikuwa hakuna daraja,” wamesema wanakijiji hao.

Kwa upande wake Mashilingi, amesema barabara hiyo itasadiis kufungua shughuli za kiuchumi husasan kwa wakulima ambao walikuwa wanashindwa kusafirisha mazao wakati wa mvua wakisubiri wakati wa kiangazi kutokana na barabara kuwa mbovu.

Mhandisi wa Ofisi ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Musoma, Mrisho Shomari, amesema ujenzi wa barabara hiyo umefanikiwa kutokana na Serikali kuongeza fedha za utekelezaji miradi ya barabara wilayani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!