May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe amshika pabaya Cyprian Musiba

Cyprian Musiba

Spread the love

 

WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, wa Tanzania, Bernard Kamilius Membe, yuko mbioni kushinda shauri lake alilofungua mahakamani dhidi ya Cyprian Musiba na gazeti lake la Tanzanite. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Membe amefungua shauri hilo la madai dhidi ya Musiba, katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Anamtuhumu Musiba, kumchafua na kumvunjia hadhi yake.

Kwa mujibu wa rekodi zilizopo mahakamani, kesi hiyo, itaanza kusikilizwa upande mmoja, kuanzia tarehe 24 Juni 2021, mbele ya Jaji Joaquine De- Mello.

Bernard Membe

Jaji De-Mello, ametoa uamuzi huo baada ya mawakili wa Membe, kutaka utekelezaji wa uamuzi wa mahakama, kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

Mahakama Kuu, imempa siku saba mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti hilo wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya Membe anayetaka kulipwa Sh. 10 bilioni.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumamosi, tarehe 22 Mei 2021

error: Content is protected !!