Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Balile mwenyekiti mpya TEF
Habari Mchanganyiko

Balile mwenyekiti mpya TEF

Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Spread the love

 

DEODATUS Balile, amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa miaka mitano ijayo, kwa kupata kura 57 dhidi Nevile Meena ya aliyepata kura 22. Anaripoti Yusuph Katimba, Morogoro … (endelea).

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumamosi, tarehe 22 Mei 2021, mkoani Morogoro ambapo idadi ya wapiga kura walikuwa 79, hakuna kura zilizoharibika.

Uchaguzi huo umesimamiwa na mwenyekiti wa uchaguzi aliyeteuliwa kwa muda, Theophile Makunga akisaidiwa na wajumbe wengine wane.

Utaratibu ulivyokuwa; wagombea wa nafasi hiyo walitolewa nje na kisha kuitwa mmoja baada ya mwingine kumwaga sera.

Aliyeanza kuitwa mbele ya wajumbe ni Deodatus Balile ambaye alipewa dakika tano za kujieleza.

Nevile Meena

Balile aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo, aliahidi kuweka mifumo itakayokuwa wazi pamoja na usomwaji ripoti na matumizi ya jukwaa kila mwaka.

Alisema, ndani ya wiki nane, ataitisha mkutano mkuu kwa ajili ya kupanga bajeti na mwelekeo wa TEF katika siku zijazo.

Pia, atahakikisha anaibua miradi yenye lengo la kuiinua jukwaa hilo na kuwa endelevu.

Balile aliahidi kuandaa bodi ya wadhamini na kisha kusajiliwa RITA kwa ajili ya kusimamia mali za TEF.

Baada ya Balile, aliitwa Meena ambaye alisema, amekuwa kiongozi kwa miaka 12 kama katibu wa TEF.

Na kwamba, sasa anahitaji kuwa mwenyekiti ili kushirikiana na bodi kuhakikisha jukwaa linakuwa na maana pana.

“Nina dhamira ya kuunganisha wahariri ndani ya TEF ili kuwa na maanda pana.

“Ndani ya TEF kuna mgawanyiko, wahariri ndani ya jukwaa hawaaminiani, wanasemana. Tukiwa pamoja, kauli ya TEF inakuwa moja,” alisema.

Meena alisema, yupo tayari kutumwa na jukwaa na atatekeleza na kwamba, atakuwa msemaji wa kile alichotumwa na si kusema cha kwake.

“Tunahitaji mwenyekiti ambaye anaweza kufanyia kazi mawazo ya wajumbe. Nitakuwa tayari kukosolewa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!