Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee na wenzake waingia mitini, Mbowe aongoza kikao
Habari za SiasaTangulizi

Mdee na wenzake waingia mitini, Mbowe aongoza kikao

Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeanza kikao chake cha dharura, jijini Dar es Salaam, kujadili tuhuma za usaliti zinazowakabili wanachama wake 19, wakiongozwa na Halima James Mdee. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mdee ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), anatuhumiwa kwa makosa matano, likiwamo kukaidi maelekezo halali ya chama chake, usaliti, utovu wa nidhamu na kushirikiana na maadui wa chama hicho.

Mkutano huo wa siku moja, unaongozwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe. Unafanyika katika hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.

Wengine wanaoshitakiwa pamoja na Mdee, ni pamoja na pamoja na Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega;  Makamu Mwenyekiti, Hawa Mwaifunga; Katibu Mwenezi wa Bawacha, Agnesta  Lambat na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Ester Bulaya.

Wanachama wengine wanaokabiliwa na tuhuma hizo, ni Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Serengeti, Esther  Matiko; Naibu Katibu Mkuu  Bawacha (Bara), Jesca Kishoa; Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje na Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara,  Tunza Malapo.

 

Katika orodha hiyo, wapo pia aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum, mkoani Arusha, Cecilia Pareso; Sophia Mwakagenda, Naghenjwa Kaboyoka, Kunti Majala,  Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Lwamlaza, Stella Siyao, Asia Mwadin Mohamed na Felister  Njau.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho kilichoanza kilichoanza asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 27 Novemba 2020, watuhumiwa wote 19, wamegoma kuhudhuria mkutano huo.

Aidha, hadi saa 7 na dakika 40 mchana, wakati wajumbe wa CC walipotoka kwa ajili ya chakula, siyo Mdee wala wenzake hao 18, ambao wengine ni wajumbe wa kamati kuu, walionekana kwenye eneo hilo.

Msemaji wa Chadema, Tumain Makene amesema, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mbowe ataongea na waandishi wa habari.

Hata hivyo, Makene hajaeleza wazi kwa nini Mdee na wenzake hawajafika mbele ya kamati hiyo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

1 Comment

  • CHADEMA tumieni busara kuliko nguvu kipindi hiki tete kulinda uhai wa chama.Waacheni wakatie chachu ya maendeleo.
    Maendeleo hayana chama upinzani ni muhimu bungeni.Igeni Marekani je wabunge wa Republican watasusia kuingia bungeni?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!