Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo Fainali CAF, Al Ahly, Zamalek kumenyana leo
Michezo

Fainali CAF, Al Ahly, Zamalek kumenyana leo

Spread the love

LEO tarehe 27 Novemba, 2020 ndio siku inayopigwa fainali ya klabu bingwa Afrika inayozikutanisha miamba ya soka nchini Misri, klabu ya Al Ahly dhidi ya Zamalek kwenye mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Cairo, Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …. (endelea).

Mchezo huo ambao unawakutanisha vigogo hao utachezwa bila uwepo wa mashabiki kutokana kuendelea kwa zuio la watu kuingiua uwanjani baada ya kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Corona ambao uliikumba Dunia mwishoni mwa 2019.

Fainal hiyo ambao itakuwa ya 55 toka kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1965, inakutanisha klabu ambazo ni wapinzani wa karne kutokana na ubora waliouonesha kwa kipindi chote hiko.

Al Ahly ambao ni bingwa nchini Misri, walifanikiwa kuingia kwenye fainali hiyo mara baada ya kuiondoka Wydad Casablanca ya Morocco kwenye nusu fainali mara baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5-1 kwenye michezo yote miwili.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza wa nusu fainal hiyo ulichezwa nchini Morocco tarehe 17 Oktoba, 2020, Al Ahly akiwa ugenini aliibuka kwa ushindi wa mabao 2-0, huku mchezo wa pili uliochezwa jijini Cairo Misri waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kwa upande wa Zamalek wao walifanikiwa kufika hatua hii ya fainali mara baada ya kuwaondosha Raja Casablanca mabingwa wa Ligi Kuu nchini Morocco kwenye hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-1, kwenye michezo yote miwili.

Kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Morocco Zamalek aliibuka na ushindi wa bao 1-0, akiwa ugenini, huku mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Misri Zamalek waliibuka tena na ushindi wa mabao 3-1.

Mpaka kufikia hatua hii Al Ahly imecheza jumla ya michezo 14 toka hatua ya makundi na kufanikiwa kushinda kushinda mechi 10, wakienda sare michezo mitatu na kupoteza mmoja.

Huku wapinzani wao Zamalek nao wakicheza michezo 14 toka hatua ya makundi na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi 8 na kwenda sare mechi tatu na kupoteza mara tatu.

Al Ahly inaingia kwenye mchezo huu wa leo huku wakiwa chini ya kocha wao mpya, Pitso Mosimane akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mara baada ya kumtimua kocha wao Rene Weiler na kuifanikisha timu hiyo kutinga fainali ya michuano hiyo.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana 2013 kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ambapo Al Ahly alifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 akiwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani.

Tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeshawaweka wazi waamuzi wa mchezo huo, huku mwamuzi wa kati ni Mustapha Ghorbal akitokea nchini Algeria mwenye beji ya FIFA, na waamuzi wasaidizi ni Abdelhak Etchiali na Mokrane Gourari kwa upande wa mwamuzi wa akiba ni Janny Sikazwe kutoka nchini Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!