Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yazungumzia uteuzi wa Mdee na wenzake
Habari za Siasa

NEC yazungumzia uteuzi wa Mdee na wenzake

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

TUME ya taifa ya uchaguzi (NEC) imesema, majina ya wabunge wa viti maalum, kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), iliwasilishwa NEC na chama chenyewe. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

“Katibu mkuu wa Chadema aliindikia barua NEC, kuwajulisha kuhusu uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum. Hivyo, Nec imeteuwa wabunge wa Viti maalum wa Chadema, kutoka kwenye orodha yake yenyewe iliyowasilisha NEC,” imeeleza taarifa ya tume hiyo, iliyosainiwa na mkurugenzi wake, Dk. Willison Charles Mahera.

Kwa mujibu wa Dk. Mahera, Chadema kiliwasilisha majina hayo kwa barua yenye Kumb. C/HQ/ADM/20/TU/05/141 ya tarehe 20 Novemba mwaka huu.

         Soma zaidi:-

Dk. Mahera anasema, “…katibu mwa Chadema, alimuandikia barua mkurugenzi wa uchaguzi, akiwasilisha orodha ya majina ya wanachama wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa wabunge viti maalumu.”

NEC imetoa ufafanuzi huo leo Ijumaa, tarehe 27 kufuatia kuibuka kwa utata juu ya uteuzi wa wabunge hao 19, walioapishwa juzi Jumanne, wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha).

Akizungumza na waandishi wa habari, siku tatu zilizopita, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, alieleza kuwa chama chake hakikuwahi kuwasilisha majina ya wanachama wake wanaopendekezwa kuteuliwa wabunge wa viti maalumu na kuitaka NEC ieleze majina hayo.

Mnyika alihoji suala hilo siku moja baada ya wabunge hao wakiongozwa na kuapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai. Mdee na wenzake hao, 24 Novemba 2020.

Tangu kuapishwa kwa wanachama hao kuwa wabunge, chama hicho kikuu cha upinzani nchini, kimekuwa kikikana madai kuwa kimewasilisha NEC orodha ya wanachama wake.

Mbali na Mdee, wengine waliopishwa kuwa wabunge, ni wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Wengine, ni katibu mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Nusrat Hanje; katibu mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha),  Grace Tendega; makamu mwenyekiti wake, Hawa Mwaifunga; naibu katibu mkuu wa Bawacha, Jesca Kishoa  na katibu mwenezi, Agnesta Lambat.

Katika orodha hiyo, mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mtwara, Tunza Malapo; Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba,  Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Wabunge hao wanadaiwa kwenda kinyume na msimamo wa Chadema wa kutopeleka wawakilishi bungeni, wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na haki.

1 Comment

  • Mnyika aliwasihi waandishi wa habari wamuulize huyo mahera kwamba alikabidhiwa na nani fomu za hao watu? Hii itasaidia kupata jibu. Kuna kitu kimejificha hapa ktk hili sakata

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!