Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge wa zamani amtupia neno Rais Magufuli
Habari za Siasa

Mbunge wa zamani amtupia neno Rais Magufuli

Ezekia Wenje, aliyekuwa mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

EZEKIEL Wenje, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana, Mwanza, amemchana Rais John Magufuli kwamba baadhi ya mairadi anayozindua ni hewa haipo, anaandika Moses Mseti.

Wenje amesema miradi inayozinduliwa na rais Magufuli, ikiwemo ya ujenzi wa barabara na miradi ya maji na kuzungumza na wananchi kwamba ni miradi hewa kwa kuwa tayari ilishawahi kuzinduliwa na Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya nne.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, kuhusu hali ya kisiasa kwa kanda ya ziwa na Taifa kwa ujumla ikiwemo kamata kamata ya viongozi wa Chadema inayoendelea kufanywa na jeshi la Polisi nchini.

Amesema kuwa rais Magufuli na Serikali yake wamekosa mawazo mbadala ya kuwaletea wananchi maendeleo na badala yake, amendelea kuwahadaa wananchi kwa kuzindua miradi hewa ambayo tayari ilikwisha zinduliwa na watangulizi wake.

Wenje ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kanda ya ziwa Victoria, amesema kuwa maisha ya Watanzania katika kipindi hiki cha rais Magufuli yamekuwa magumu kuliko mwaka 2015, lakini anashangazwa kuona serikali ikizidi kuzindua miradi hewa na isiyokuwa na tija.

Amesema kuwa licha ya hali mbaya ya maisha kwa Watanzania, kwa kupanda gharama za maisha lakini serikali ya Magufuli imeshindwa kutambua hilo na badala yake wameendelea kuzunguka mikoani na kuzindua miradi hewa isiokuwa na faida kwa watanzania.

Wenje ameongeza kuwa miradi mingi ya maendeleo nchini inashindwa kutekelezwa kwa kuwa fedha zinazotengwa ni kidogo, huku akitolea mfano bajeti ya mwaka 2015 – 2016 fedha zilizokwenda ni chini ya asilimia 38.

“Serikali ya JPM haina mawazo mapya ya kupambana na sisi na kama wanaona wana uwezo wa kupambana na sisi watuache tufanye mikutano ya hadhara kwa kuwa wanafahamu mabaya yao wanayoyafanya,” anasema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!