Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Biashara Mbunge Lugangira azindua kampeni ya “Pika na Gesi”
Biashara

Mbunge Lugangira azindua kampeni ya “Pika na Gesi”

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum CCM, Neema Lugangira amezindua Kampeni ya “Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira” inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo amegawa mitungi 300 ya gesi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Lugangira amezindua kampeni hiyo jana Alhamis wilayani Bukona mkoani Kagera ambapo ameweka wazi kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo aliyotoa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika Novemba Mosi 2022, mkoani Dar es Salaam.

Mbunge huyo amesema kuanzia ametoa mitungi 300 ya gesi kwa viongozi wa makundi mbalimbali, wajasariamali, mama lishe na Wwatu mashuhuri katika Wilaya ya Bukoba mjini mkoani humo.

Amesema Kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira imeanzishwa na kuratibiwa na ofisi yake kupitia Neema na Maendeleo na Shirika la Agri Thamani.

“Kampeni hii imeanzia Wilaya ya Bukoba ikifuatiwa na Wilaya ya Muleba na baadae itafika maeneo mengine ndani na nje ya Mkoa wa Kagera kulingana na uwezeshwaji utakaopatikana,” amesema.

Mbunge Lugangira ameishukuru Wizara ya Nishati kwa kuwapa semina wabunge kuhusu umuhimu wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia na uwezeshwaji uliofanikisha uzinduzi huu.

Aidha, Lugangira ameshukuru Jamilla Haroub, Mratibu wa REA Bukoba na Masota Mafuru, Ofisa Masoko Oryx Gas Mkoa wa Kagera na Geita kwa ushirikiano mkubwa waliompatia.

Mbunge huyo ambaye amekuwa akipambana kutatua changamoto za jamii, amewakaribisha wadau wengine kumuunga mkono kufanikisha Kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira ili kufikia makundi mengine kwenye jamii kwa lengo la kulinda afya za wakina mama, kutunza mazingira na kuepusha madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, mambo ambayo yatapelekea kuimarisha lishe bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita

Spread the loveMAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

Biashara

TPHPA yafunda wafanyabiasha, wakulima matumizi ya viuatilifu

Spread the loveMAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imetoa...

error: Content is protected !!