Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Kubenea alia na rafu za serikali ya JPM
Habari za Siasa

Mbunge Kubenea alia na rafu za serikali ya JPM

Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema Watanzania wanakuwa maskini kwa sababu ya ubaguzi unaofanywa na serikali, anaandika Hellen Sisya.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika eneo la Kimara Kilungule,

Mbunge huyo alisema kuwa  serikali imekuwa ikibagua shughuli za maendeleo.
Amesema serikali imeshindwa kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo kwa maeneo ambayo yanaongozwa na wapinzani.

Ametoa mfano kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita kwamba  mradi huo haukuwa na ulazima wowote kwani serikali ilikuwa na uwezo wa kuuboresha uwanja wa ndege uliopo jijini Mwanza badala ya kujenga mwingine.

“Ni lazima nchi hii iache upendeleo, iache ubaguzi, viongozi ni lazima wawe mfano kwa wananchi, ukianza kubagua hawa wapinzani, hawa ni CCM, ndani ya wapinzani wanaishi CCM, ndani ya CCM wanaishi upinzani.” amesema Kubenea.

Aidha, Mbunge huyo alisema ni lazima serikali iache kuwalinda baadhi ya watu ili kuleta usawa mbele ya sheria badala ya kuangalia sura wala cheo cha mtu.

“Mwalimu Nyerere alituacha tukiwa wamoja, taifa hili limeachwa likiwa moja, leo linakatwa vipande vipande kwa chuki na uhasama usio na msingi. Kuna ubaguzi kwenye nchi.!!Mtu mmoja,wamefanya makosa pamoja, mmoja anapelekwa mahakamani, mwingine ameachwa .” amesisitiza Mbunge huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!