May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM alia ukata vituo vya Afya Segerea

Bonna Kamoli, Mbunge wa Segerea

Spread the love

 

BONNA Kamoli, Mbunge wa Segerea, jijini Dar es Salaam (CCM), ameihoji Serikali, lini itaongeza vituo vya afya katika jimbo hilo, ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa huduma za afya kwa wananchi wake. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Kamoli amehoji hayo leo Jumatano tarehe 28 Aprili 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo wa Segerea amesema, wananchi wa kata 13 katika jimbo hilo wanatumia kituo cha afya kimoja.

Na kuhoji lini Serikali itapandisha hadhi Zahanati za Kinyerezi, Segerea, Kipawa na Yombo Kiwalani, ili kuondoa adha hiyo.

“Je, ni lini Serikali itaongeza Vituo vya Afya katika Kata za Jimbo la Segerea ikiwemo kupandisha hadhi Zahanati za Kinyerezi, Segerea, Kipawa na Yombo Kiwalani ili kuondoa adha kwa Wananchi wa Kata 13 wanaotegemea Kituo kimoja cha Afya?” Amehoji Kamoli.

Sambamba na hilo, Kamoli amehoji lini Serikali itajenga Zahanati katika Kata za Minazi Mirefu, Buguruni, Kimanga na Kisukuru.

“Je, ni lini Kata za Minazi mirefu, Buguruni, Kimanga na Kisukuru zitapatiwa Zahanati?” amehoji Kamoli.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk. Festo Dugange, amesema, katika mwaka wa fedha ujao (2021/22), Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga Sh. 1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vitatu, pamoja Sh. 2.7 bilioni kwa ajili ya kupandisha hadhi zahanati tano.

Naibu waziri huyo wa Tamisemi amesema, mpango huo utanufaisha Segerea, kwa kuwa kiasi cha fedha hizo kitatumika kuongeza miundombinu ya Zahanati za Kinyerezi na Kiwalani, zilizomo katika jimbo hilo, kwa ajili ya kuzipandisha hadhi kuwa vituo vya afya.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani imetenga Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya na Shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya kuongeza miondombinu katika Zahati tano.

Iili ziweze kupandishwa hadhi kuwa Vituo vya Afya zikiwemo Zahanati za Kinyerezi na Kiwalani katika Jimbo la Segerea,” amesema Dk. Dugange.

Kuhusu kata zisizokuwa na Zahanati, Dk. Dugange amesema Serikali imetenga Sh. 250 milioni kwa ajili ya kukamilisha maboma matano ya zahanati katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, zikiwemo zahanati za Bonyokwa na Tabata ziliko katika jimbo hilo.

error: Content is protected !!