Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge awashambulia mawaziri wa Rais Magufuli
Habari Mchanganyiko

Mbunge awashambulia mawaziri wa Rais Magufuli

Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga (katkati) akiwa bungeni na wabunge wenzake wa upinzani
Spread the love

MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) leo aliwashambulia mawaziri wa Rais Magufuli kwa kueleza kuwa majibu yao asilimia kubwa ni ya uongo, anaandika Dany Tibason.

Mwita ameelekeza mashambulizi hayo leo bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kudai kuwa majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliani, Isack Kamwelwe ni asilimia tano tu ya swali lake na asilimia 95 ni uongo.

“Mimi ni mwalimu wa hisabati na kemia nimekuwa nisahihisha mitiani ya serikali na kama ningekuwa nasahisha mitihani ya mawaziri wewe ningekupa asilimia tano tu kati ya mia majibu niliyouliza imejibiwa asilimia tano tu yaliyobaki ni uongo.

“Inaonesha waziri hauna taarifa sahihi ya miradi ya maji ya kata nilizozitaja katika swali la msingi Je, huko tayari sasa uniletee taarifa sahihi.

“Je, kwa sasa hupo tayari nikukutanishe na akina mama ambao wanakumbana na adha ya kutafuta maji na kulazimika kununua maji kwa sh. 500 kwa ndoo ili uweze kusikiliza kilio chao juu ya kukosekana kwa maji?” alihoji Waitara katika swali lake la nyongeza.

Awali katika swali la msingi Waitara alitaka kujua serikali itakamilisha lini miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe ili wananchi wa kata hizo na maeneo ya jirani wapate maji ya uhakika.

Pia mbunge huo alitaka kujua ni lini serikali itachimba bwawa kubwa katika mnada wa kimataifa ili ng’ombe wanaouzwa ili wapate maji.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe, amesema serikali inakamilisha miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe.

Amesema miradi mingi imekamilika na inawahudumia wananchi na mingine hipo katika hatua nyingine za ujenzi, miradi iliyokamilika ni pamoja na Kipungunguni ‘B’ kwa Mkoremba, Chanika shuleni, Majohe, Nyang’andu na Msongola.

Kamwelwe amesema serikali imepanga kupeleka maji katika maeneo ya Pugu kutoka katika miradi mkubwa wa visima virefu vilivyopo mpera katika wilaya ya Mkuranga na kazi ya uchimbaji wa visima inaendelea na matarajio ya kukamilisha uchimbaji katika mwaka huu wa fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!