Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheria ya ndoa kurekebishwa kumaliza ndoa za utotoni
Habari Mchanganyiko

Sheria ya ndoa kurekebishwa kumaliza ndoa za utotoni

Dk.Hamisi Kigwangalla, waziri wa Maliasili na Utalii
Spread the love

SERIKALI imesema ipo haja ya kuondoa vifungu vinavyoruhusu ndoa za utotoni kwenye sheria ya ndoa kwa lengo la kumlinda mtoto wa kike na ndoa za utotoni, anaandika Dany Tibason.

Dk. Khamis Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alioa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Faida Bakari Mohamed (CCM).

Faida alitaka kujua ni sheria zipi zinazowanyima haki wanawake na watoto nchini na lini serikali itapeleka miswada Bungeni ili kuboresha au kubadilisha Sheria hizo ili ziendane na wakati na kuwapatia haki zao Wanawake na watoto.

Dk. Kigwangallah amesema katia jitihada za kutokomeza ndoa za utotoni mwaka 2016 serikali ilifanyia marekebisho sheia ya elimu ya mwaka 1978 ili kuzia watoto wa shule wasiolewe.

“Kwa mujibu wa Sheria hii Na. 4 ya mwaka 2016 kifungu cha 60A, hairuhusiwi mtu yeyote kuoa ama kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari,” amesema Dk. Kigwangallah

Adha amesema sheria ambazo zimekuwa zikiwanyima haki za urithi ni pamoja nashetia za mirathi za kimila za mwaka 1963 zimekuwa zikiwanyima haki za urithi na umiliki wa ardhi wanawake na watoto.

“Vile vile Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 katika kifungu cha 13 na 17, vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo wa miaka 14 au 15 kwa ridhaa ya wazazi au mahakama, vifungu hivi pia humnyima mtoto haki za msingi,” alisisitiza.

Katika swali la nyongeza Faida aliihoji serikali kwamba kwa nini isiitambue Mahakama ya Kadhi kama chombo cha waislamu katika masuala ya ndoa ili kuokoa Sheria za kiislam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!