Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mashine ya Mil 100 yatoweka Mpanda
Habari Mchanganyiko

Mashine ya Mil 100 yatoweka Mpanda

Mashine ya kusaga na kukoboa
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum Rhoda Kunchela (Chadema) ameitaka serikali kufuatilia na kutoa taarifa juu ya matumizi mabaya ya mashine ya kukoboa na kusaga ambayo ilinunuliwa kwa zaidi ya Sh. 100 milioni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri ya Mpanda, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo, mbunge huyo amesema serikali itoe kauli juu ya matumizi mabaya ya mashine ya kukoboa na kusaga ambayo ilinunuliwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri ya Mpanda.

“Kwa kuwa nchi bado inakabiliwa na upungufu wa viwanda na kunasera ya kuifanya nchi kuwa ya viwanda, serikali inatoa kauli gani juu ya ununuzi wa mashine ya kukoboa na kusaga ambayo ilinunuliwa na halmashauri ya Mapanda kwa zaidi ya Sh. 100 milioni, lakini kwa sasa mashine hiyo haijulikani ilipo na jengo lililojengwa kwa ajili ya kuweka mashine hiyo limekuwa gofu.

“Je kutokana na hali hiyo serikali inatoa kauli gani ili kuhakikisha mashine hiyo inarejeshwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokusudiwa na Je, waziri wa viwanda yupo tayari kufika katika halmashauri ya Mpanda ili kuweza kubaini ni wapi ilipo mashine hiyo ili iweze kutumiwa kwa matumizi yaliyokusudiwa,” amehoji Kuchela.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Lucia Mlowe, (CCM) alitaka kujua kama serikali ipo tayari kujenga kiwanda cha chai kunusulu uchumi wa wakulima wa chai katika wilaya ya Njombe.

“Mgogoro wa kiwanda cha chai cha Lupembe na wilaya nzima ya Njombe kutokana na kukosa soko la zao la chai.

“Je serikali ipo tayari kujenga kiwanda kingine cha chai kunusuru uchumi wa wakulima wa chai katika wilaya ya Njombe,” amehoji Mlowe.

Akijibu maswali la nyongeza la Kunchela, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo atafanya ziara katika mikoa ya Rukwa na Katavi pamoja na kufuatilia mashine hiyo ili iweze kujulikana ni wapi ilipo na inafanya nini.

Akijibu swali la msingi Mwijage amesema serikali inatambua umuhimu wa kuwa na viwanda vya kutosha ili kuchochea kilimo cha zao la chai na usindikaji wa majani ya chai katika mkoa wa Njombe na serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika mkoa huo.

Aidha amesema kampuni ya Unilever imeanza ujenzi wa kiwanda kipya cha chai na kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwaka kesho na kutoa ajira zaidi ya 300, mwekezaji anatarajia kuanzisha mashamba ya chai yenye ukubwa wa hekari 1,000 kati ya hizo hekari 200 zimeisha pandwa mbegu ya chai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!