March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge aliyetishia kuhamia CCM, ahamia kweli

Spread the love

MBUNGE wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha amejiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza leo Septemba 27, 2018 Chacha amesema amechukua uamuzi huo kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Amesema wakati akigombea ubunge aliahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini dhamira yake haijafanikiwa kutoka na vikwazo anavyokumbana navyo ndani ya Chadema.

Chacha amewataka wakazi wa Serengeti kumchagua mtu atakayeweza kushirikiana nao pamoja ili kuleta maendeleo kupitia CCM.

Mbunge huyo alikutana na wakati mgumu wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani Mara ya kuzomewa na wananchi alipobanwa na maswali.

Baada ya kuzomewa Chacha alipopata nafasi kuzungumza alisema, wanamzomea kwa sababu yeye siye CCM lakini ipo siku naye atakuwa CCM.

error: Content is protected !!