March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

MV Nyerere sasa yaelea Ziwa Victoria

Spread the love

JUHUDI za unyanyuaji meli ya MV Nyerere zimefikia hatua nzuri baada ya kuinuliwa na kuanza kuonesha taswira yake ya siku zote. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo ni mafanikio ya wataalam na waokoaji wakiongozwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Harakati za kunyanyua kituo hicho mpaka kufikia mwonekano mzuri wa sasa umechukua siku tano.

Tangua kuanza juhudi za kunyanyua meli hiyo, mbinu mbalimbali zimetumika ikiwa ni pamoja na kutumia greda kuvuta waya uliofungwa kwenye meli, kupitisha mabomba na kisha kujaza upepo.

Wataalam wanaendelea kumalizia kazi hiyo na kisha itakabidhiwa rasmi kwa serikali.

MV Nyerere ilizama tarehe 20 Septemba mwaka huu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 220 na mali nyingi kupotea.

error: Content is protected !!