May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge alilia deni bilioni 5 la wananchi, Bashe amjibu

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo

Spread the love

 

ISSA Mchungahela, mbunge wa Lulindi (CCM), mkoani Mtwara, ameiomba Serikali ya Tanzania, kuwalipa wananchi wanaodai miche ya mikirosho, deni ambalo lina muda la mwaka 2017. Anaripoti Jemima Samwel DMC …(endelea).

Ameyasema hayo leo Jumatano, tarehe 2 Juni 2021, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo amesema, deni hili ni la muda mrefu tangia mwaka 2007.

“Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi wanaodai miche ya mikorosho deni ambalo ni la muda mrefu tangu mwaka 2017?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, katika msimu wa mwaka 2017/2018, Serikali kupitia Bodi ya Korosho, iliingia mikataba na wazalishaji wa miche 678 ili kuzalishamiche 13,661,433 ya korosho yenye thamani ya Sh.5.31 bilioni

“Jumla ya miche 12,298,927 sawa na asilimia 92 imesambazwa kwa wakulima katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani, Tanga, Singida, Tabora, Dodoma, Kilimanjaro, Morogoro, Njombe,Mbeya, Iringana Songwe,” amesema

Aidha, malipo kwa wazalishaji hao yamechelewa kutokana na zoezi la uhakiki kuchukua muda ili kujiridhisha kabla ya kufanya malipohayo.

“Kutokana na uhakiki umefanywa katika awamu ya kwanza na timu ya wataalamu kutoka serikalini, jumla wazalishaji miche 382 waliozalishamiche 5, 858, 979 yenye thamani ya Sh.2.37 bilioni wameshalipwa.”

“Kupitia uhakikiwa awamu ya pili uliofanyika mwezi Agosti hadi Oktoba 2020, ulibaini jumla ya miche 5,815,519 yenye thamani ya Sh.2.66 bilioni ilihakikiwa nabadokulipwa,” amesema amesema Bashe .

Bashe amesema, Serikali inakamilisha taratibuza malipo kwawazalishaji hao wa miche.

error: Content is protected !!