KLABU ya Simba kesho itashuka Uwanjani kumenyana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, Mwanza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 11 jioni ambapo utakuwa mchezo wa mwisho kwa simba kabla ya Ligi hiyo kwenda mapumziko kwa wiki mbili kupisha kambi ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wanaoingia kambini kuanzia tarehe 5 Juni, 2021.
Kikosi hiko cha Simba kilitua Jijini Mwanza jana kwa ajili ya mtanange huo ambao kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa tarehe 26 Oktoba, 2021 kwenye Uwanja wa Simba ilipoteza kwa bao 1-0.

Simba inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kupata mataokeo ya ushindi wa mabao 3-1, mbele ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo wilaya ya Ruangwa, Lindi.
Mabingwa hao watetezi kesho wataendelea kukosa huduma ya kiungo wao Clatous Chama ambaye yupo nchini Zambia mara baada ya kufiwa na mke wake.
Wenyeji wa mchezo huo Ruvu Shooting wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa kwenye nafasi ya 10 na pointi 37 mara baada ya kucheza michezo 29.
Simba wao bado wamesalia kileleni wakiwa na pointi zao 64, mara baada ya kucheza michezo 26 huku wakilisaka taji la nne la Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.
Leave a comment