Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe yupo fiti, atinga mahakamani
Habari za Siasa

Mbowe yupo fiti, atinga mahakamani

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amefika leo tarehe 31 Januari, 2019 kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi inayomkabili yeye na viongozi waandamizi wa chama hicho akionekana mwenye afya njema. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe na viongozi waandamizi wengine wanane wa chama hicho wanashtakiwa kwa kufanya mkusanyiko na maandamano yanayodaiwa kuwa siyo halili.

Tarehe 17 Januari 2019  Mbowe alishindwa kuhudhuria mahakamani hapo kwa kilichoelezwa na upande wa mashataka  kuwa anaumwa.

Mbowe  na Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini ambao wamefutiwa zao dhamana tangu Mwezi Novemba mwaka jana kwa kilichotajwa kuwa amekwenda kinyume na mashaart ya dhamana.

Viongozi wengine wanaoshitakiwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Z’bar, John Mnyika, Mbunge Naibu katibu Mkuu Bara, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, Mch. Peter  Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini.

Leo mbele ya Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina ambaye amepokea kesi hiyo kwa aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Wakili wa serikali Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa kesi hiyo imefika kwa ajili ya kutajwa mpaka pale rufaa ya dhamana iliyoombwa na upande wa utetezi mahakama kuu itakaposikilizwa.

Baada ya maelezo hayo wakili wa upande wa utetezi, Profesa Abdallah Safari ameieleza mahakama hiyo kuwa rufaa itasikilizwa tarehe 18 Februari mwaka huu.

Hakimu mhina ameihalisha kesi hiyo na kuitaja tena tarehe 14 Februari mwaka huu.

Viongozi hao wanashtakiwa mahakamani hapo kwa makosa 13 pamoja na kula njama  ya kufanya ghasia, kufanya maandamano kinyume cha sheria, kuhamasisha chuki, kufanya uchochezi na wanadaiwa kutenda makosa hayo terehe 1 na 16 Februari mwaka 2017.

https://www.youtube.com/watch?v=S9VOZ4NOC0g&feature=youtu.be

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!