Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Michezo Kichuya kutimkia Misri
Michezo

Kichuya kutimkia Misri

Spread the love

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya huenda akatimka ndani ya klabu yake muda mchache ujao na kujiunga na timu ya Pharco inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …  (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba inaeleza kuwa wapo katika mazungumzo ya mwisho na Pharco kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo ili aweze kujiunga na timu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

“Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya nchini Misri kuhusu mchezaji Shiza Kichuya kwenda kujiunga na timu hiyo. Taarifa zaidi itatolewa baadae baada ya taratibu zote kukamilika.”

Kichuya alijiunga na Simba 2015 akitokea klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na kufanikiwa kucheza misimu minne ndani ya katika kikosi cha kwanza huenda akawa msaada mkubwa kwa klabu yake mpya.

Endapo mchezaji huyo atafanikiwa kujiunga na klabu hiyo atakuwa ameongeza idadi ya wachezaji kutoka Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi kama Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva, Himid Mao, Rashid Mandawa, Said Chilunda, Abdi Banda, Hassan Kessy na Eliud Ambokile.

 

 

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

Michezo

Yanga SC. yatwaa ubingwa wa pili mfululizo

Spread the love  KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa...

error: Content is protected !!