Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe Vs Jamhuri: Neno kwa neno
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe Vs Jamhuri: Neno kwa neno

Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani
Spread the love

SHAHIDI wa tano kwenye kesi namba 112 ya mwaka 2018 ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, hajui kilichomfanya askari mlenga shabaha (Koplo Rahimu) azimie. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Shahidi huyo aliyejitambulisha kuwa ni daktari kwenye Hosptali ya Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa. Jijini Dar es Salaam ndiye aliyewapokea askari wawili waliodaiwa kujeruhiwa kwenye maandamano ya wafuasi wa Chadema Kionondoni, Mkwajuni.

Jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba shahidi huyo alijitambulish kuwa ni Tabibu Msaidizi (Assistance Medical Officer) kwenye hospitali hiyo.

Upande wa serikali uliwakilishwa na mawakili waandamizi wa serikali Faraja Nchimbi, Paul Kadushi, Wankyo Simon na Salim Msemo. Kwa upande wa utetezi uliongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Yafuatayo ni mahojiano ya shahidi huyo na mawakili wa utetezi, Kibatala baada ya upande wa serikali kumaliza kumhoji.

Kibatala:  Bahati mzuri mimi nimekulia katika familia ya madaktari, unafahamu kuwa kuna mgawanyiko wa aina sita za wananchama wanaosajiliwa na baraza na madaktari Tanzania?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu kuwa hakuna mtoa huduma holela asiyetambuliwa na baraza?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Unafahama kwamba, hata madaktari wanaosoma pale Muhimbili ni wanachama hata kama hawajamaliza mafunzo yao?

Shahidi: Hilo sifahamu.

Kibatala: Unamfahamu Rais wa Baraza la Madaktari Tanganyika? Kwa mfano itakuwa ajabu kwa wakili kutomjua rais wake?

Shahidi: Nimesahau.

Kibatala: Mwambie hakimu, nyaraka gani tano za usajili kwenye baraza la madaktari?

Shahidi: Nafahamu moja.

Kibatala: Tutaamini vipi kama wewe umesajiliwa?

Kibatala: Umesema MAO umeipata chuo gani?

Shahidi: Chuo cha Lugalo

Kibatala: Mwambie hakimu, daktari aliyekusimamia pale Lugalo wakati unasoma?

Shahidi: Nimesahau

Kibatala: Mwambie hakimu Mkuu wa Chuo cha Lugalo wakati wewe unamaliza mafunzo yako?

Shahidi: Dk Simon.

Kibatala: Dk Simon nani?

Shahidi: Jina la pili nimesahau.

Kibatala: Hivi shahidi hospitali kama Lugalo inaongozwa na daktari wakati mimi najua Head wa hospitali alikuwa Profesa?

Kibatala: Ni kawaida Hospitali kubwa kama Lugalo iongozwe na Daktari tu?

Shahidi: Inawezekana.

Kibatala: Tofauti kati ya Daktari na Assistance Medical Officer?

Shahidi: Madaraka.

Kibatala: mtu anayeitwa daktari na msaidizi wa daktari tofauti yake nini?

Shahidi: Level unayosomea.

Kibatala: Level unayosomea manaake nini?

Shahidi: Level ni kusomea ofisa.

Kibatala: Ndio maana nilikuambia kuwa nimekulia katika mazingira ya udaktari Medical Oficer anakuwa ana degree?

Shahidi: Sio sahihi.

Kibatala: Unafahamu kuwa hapa mahakamani tuna madaktari hata mshitakiwa Mashinji ni MD, tuambie Medical Doctor kwa ushahidi wako ni sahihi.

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ni sahihi kuwa MAO haruhusiwi kufanya baadhi ya upasuaji?

Shahidi: Sio sahihi anaruhusiwa inategemea na udhoefu wake.

Kibatala: Shahidi twende pale Kilwa Road, Polisi Hospitali …Umeongozwa kusema chochote kuwepo kwa MD, au mpasuaji?

Shahidi: Sijasema.

Kibatala: Narudia swali langu uliongozwa kusema chochote kuhusu mpasuaji au wapasuaji?

Shahidi: Sikumbuki.

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusiana na kuwepo kwa MD au MDs pale Kilwa Road Hospital?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusiana na Physiotherapist?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusu kitengo cha upasuaji au hata chumba cha upasuaji?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Ni sahihi kuwa wewe ni daktari msaidizi?

Shahidi: Usitafsiri kwa tafsiri hiyo.

Kibatala: Ni sahihi kuwa wewe Boss wako ni Medical Doctor ni sahihi kuwa, wewe Medical Assistance ni daktari msaidizi?

Shahidi: Sijaelewa swali.

Kibatala: Shahidi nakuuliza tushakubaliana kuna mtu Specialist, huyu mtaalamu na kuna mtu anaitwa Medical Doctor na kuna mtu anaitwa Medical Assistance Officer haruhusiwa kutumia hata neno Doctor?

Shahidi: Sio sahihi ni daktari.

Kibatala: Kuna mtu anaitwa Nurse Officer na kuna mtu anaitwa Nurse Assistance anaitwaje kwa Kiswahili?

Shahidi: Anaitwa Nurse?

Kibatala: Ni Sahihi Nurse Assistance ni msaidizi?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Unasema Nurse alikuja kukuita ulipokuwa kwenye wodi ya wazazi saa tano na dakika 40?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ni kwanini unakumbuka muda mahususi wa wewe ukumbuke siku ile saa tano na dakika 40, nini hasa kimekufanya ukumbuke?

Shahidi: Kwa sababu ya hii kesi na nakumbuka majina ya hao watu nakumbuka niliwahudumua.

Kibatala: Kwanini unakumbuka muda mahususi au jibu lako litakuwa kuhusu hii kesi?

Shahidi: Kimya.

Kibatala: Unakumbuka siku hiyo ulihudumiwa wagonjwa wangapi?

Shahidi: Wanne.

Kibatala: Hawa wengine unakumbuka uliwahudumia saa ngapi?

Shahidi: Nakumbuka.

Kibatala: Ili kuweka ukweli kama hii sio hadithi ya kutunga kama kweli unakumbuka uliongozwa kuwataja hawa wagonjwa wengine?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Unakumbuka kuongozwa kutaja madaktari wengine?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Uliongozwa kutaja mtu au watu waliowaleta hao majeruhi?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Shahidi unasema hawa wahanga wawili walikuwa conscious (wanajitambua) ..unaelewa maana ya consious

Shahidi: Sio kweli.

Kibatala: Sio kweli nini?

Shahidi: Sio sahihi.

Kibatala: Nataka umwambie Hakimu yupi hakuwa Consious (kujitambua)?

Shahidi: Koplo Rahimu.

Kibatala: Maana yake ni kwamba mpaka unamuhudumia Koplo Rahimu alirejea kwenye fahamu mbele yako?

Hakimu Simba: Jibu swali.

Shahidi: Mbele yangu.

Kibatala: Kwa ushahidi wako Koplo Rahimu mpaka unamuhudumia alikuwa hajitambui na ulisema kuwa, saa tatu ulikuwa muda wa madhara sasa wewe haya masaa matatu alikuambia nani ikiwa Rahimu alikuwa hajitambui?

Shahidi: Rudia swali.

Kibatala: Aliyekupa taarifa juu ya huyu mgonjwa aliyekuja akiwa hajitambui ilhali imeandika muda wa madhara ni saa tatu alikuambia nani?

Shahidi: Sikuambiwa na mtu yoyote.

Kibatala: Rahimu alijitambua saa ngapi?

Shahidi: Saa 5 na dakika 50.

Kibatala: Na wewe ulimfikia Rahimu na kuanza kumtibai saa ngapi?

Shahidi: Saa 5 na dakika 50.

Kibatala: Alijitambua wakati wewe unafika au ulichukua muda?

Shahidi: alichukua muda.

Kibatala: Kama dakika ngapi?

Shahidi: Dakika tano.
Kibatala: Wakati jibu la mwisho linarekodiwa mbele yako kuna mgonjwa amezimia nini cha kitabibu kinafanyika?

Shahidi: Huduma ya kwanza.

Kibatala: Ipi?

Shahidi: ABCD una hakika mapigo ya moyo na upumuaji?

Kibatala: Mwambie hakimu kama uliongozwa kusema hizo ABCD?

Shahidi: Sijaongozwa

Hakimu Simba: Unasema.

Shahidi: Nilihakiki mfumo wa upumuaji na mapigo ya moyo.

Kibatala: Ulivyongozwa uliyasema hayo?

Shahidi: Sikuyasema lakini niliamuru manesi wameweke Dripu.

Kibatala: Uliongozwa kuwataja hao manesi idadi yao na majina yao?

Shahidi: Kwanza rekebisha kauli yako mimi siongozwi.

Kibatala: Sio ugomvi kuongozwa ni neno la kisheria tunalotumia hapa mahakamani ndio maana hawa mawakili wenzengu hawakupinga.. uliongozwa au hukuongozwa?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Mgonjwa aliwekewa drip ya aina gani gani?

Shahidi: Zipo nyingi.

Kibatala: Wakati unatoa ushahidi wako uliitaja aina na kazi yake?

Shahidi: Sikutaja aina.

Kibatala: Na hata kazi yake hukutaja?

Shahidi: Kazi sikutaja.

Kibatala: Shahidi mpaka leo unatoa ushahidi hapa unafahamu ni kwanini Koplo Rahimu amezimia?

Shahidi: Sijui chochote.

Kibatala: Nani anajua?

Shahidi: Anajua mwenyewe.

Kibatala: Kwa hiyo wewe daktari hufahamu sababu ya Mgonjwa kuzimia?

Shahidi: Rudia kuniuliza.

Kibatala: Unafahamu chanzo cha Koplo Rahimu sababu ya kitabibu?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Sasa wewe umekuja hapa kama mtaalamu unasema hujui?

Shahidi: Sijui labda za kitalamu.

Kibatala: Ndio nayotaka ni sababu?

Shahidi: Ni ukosefu wa Oxygen kwenye Ubongo.

Kibatala: Sasa ni wapi kwenye kielelezo P1 ulichokitoa wewe ni wapi umeandika kuzima kwake kumesababishwa na ukosefu wa Oxygen?

Shahidi: Haipo.

Kibatala: Hivi ni kweli ukosefu wa Oxygen unaweza kusababisha majeraha ya ubongo?

Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ni wapi uliandika kuwa anatakiwa kufanyiwa uchunguzi kwenye ubongo?

Shahidi: Sijaandika.

Kibatala: Uliamrisha kufanyiwa uchunguzi wa CT-Scan kwa Klopo Rahimu?

Shahidi: Sio kweli sikuamuru kwa ajili ya kuchunguza majeraha ya ubongo.

Kibatala: Ukifanyiwa uchunguzi wa CT-Scan kuna Ripoti inakuja?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ambayo hiyo umeitoa kama Kielelezo?

Shahidi: Sijatoa.

Kibatala: Ulizungumzia chochote kuhusu hayo majibu?

Shahidi: Kama ilifanyika siwezi kujua ..Najibu nilichofanya.

Kibatala: Wewe ndio uliojaza PF3 ukashauri juu ya CT-Scan ni nani anatakiwa kufahamu juu ya CT-Scan?

Shahidi: Mgonjwa ndio anatakiwa kujua mimi nilishamaliza najibu nilichofanya.

Kibatala: Ni sahihi mpaka tarehe 20 ulikuwa hujui kutimizwa kwa haya uliyashauri CT-Scan au Phisiotherapist?

Shahidi: Nilikuwa sijui.

Kibatala: Wakati unaongozwa je ulisema chochote kufafanua Antibiotics ni nini?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Ni sahihi au nilikusikia vibaya kuwa Koplo Rahimu zaidi ya kidonda cha shingoni alikuwa anakidonda kingine?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwa ushahidi wako wewe mwenyewe Koplo Rahimu alizimia na alizinduka saa 5 na 50, ulizungumzia chochote uliipataje hii PF3 ambayo inaonesha uliijaza saa 5 na dakika 50 ?

Shahidi: Kimya.

Kibatala: Kwa ushahidi wako wewe mwenyewe Koplo Rahimu alizimia na alizinduka saa 5 na 50, ulizungumzia chochote uliipataje hii PF3 ambayo inaonesha uliijaza saa 5 na dakika 50, Je ulizungumza chochote namna PF3 hii ilivyokufikia wewe?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Wewe ni Ofisa wa Polisi, PF3 inapaswa kubebwa na nani?

Shahidi: Majeruhi

Kibatala: Ni sahihi kwamba, mtu wa tatu anaruhusiwa kuibeba?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ulimtaka mtu mwengine uliyekuwa naye wakati Rahimu yupo Hospitali?

Shahidi: Nilikuwa na Staff wenzangu.

Kibatala: ulitaja majina ya Daktari aliyemruhusu Koplo Rahimu?

Shahidi: Sikumtaja.

Kibatala: Nani anayetakiwa kumiliki hati ya kuruhusiwa kwa Mgonjwa na ni sahihi kuwa Koplo Rahimu ndio mwenye hiyo hati?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Kwa utaratibu wa hospitali kuna faili fulani linalozungumzia taarifa za mgonjwa, na wewe kwa vile uliwahi kumuhudimia ni sahihi kuna mahali ulijaza?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Mwambie Hakimu iwapo wewe hilo faili umelitoa mahamakani na kumwambia hakimu kuwa nilijaza hapa na hapa?

Shahidi: Sijatoa.

Kibatala: Ni sahihi kwamba pale Hospitali kuna usajili kama aidha anaufanya mgonjwa mwenyewe au mhudumu anamsaidia endapo hajiwezi?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Umetoa kielelezo chochote kama kweli kuhusu kusajiliwa kwa Koplo Rahimu?

Shahidi: Sijatoa.

Kibatala: Ni tathimini yako kuwa Koplo Rahimu alizima muda wa saa 5 kabla ya kuzinduka mbele yako?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Kuna kanuni yoyote ya kitabibu kwamba kuna hospitali nyengine mgonjwa au ni lazima apeelekwa hospital ya Kilwa Road?

Shahidi: Popote anaweza kupelekwa.

Kibatala: Mtu akizimia mfano mimi nimezima hapa kutoka na majibu yako nikazimia ni lazima nipelekwe Kilwa road?

Shahidi: Inategemea mimi siwezi kuamua.

Kibatala:Tturejee kwa bwana Fikiri ulisema alikuwa anavuja damu

Shahidi: Alikuwa akivuja damu

Kibatala: Nilikusikia sahihi kwamba huduma ya kwanza aliipata pale chumba cha dharura?

Shahidi: Nilisema alipelekwa chumba kwa ajili ya kufungwa bandeji.

Kibatala: Ni sahihi bandeji ya kwanza uliifunga wewe?

Shahidi: Niliifunga mimi.

Kibatala: Ni sahihi bwana Fikiri alipata majareha saa 12 na 32 jioni?

Shahidi: Hiyo mimi sijui.

Kibatala: Hiyo PF3 imefikaje?

Shahidi: Alikuwa ameishika mkononi.

Kibatala: Ulimuuliza ameipataje.

Shahidi: Sijamuuliza.

Kibatala: Shahidi nini madhara ya mtu kuvuja damu kwa muda mrefu?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Nini madhara ya damu kutoka muda mrefu?

Shahidi: Kuzimia.

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusu kumuongezea damu PC Fikiri?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Shahidi katika kielelezo chochote ulijaza mahala popilote kuhusiana kuongezwa damu PC Fikiri?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Huyu PC Fikiri ni nani aliyemshona?

Shahidi: Ni mimi.

Kibatala: Ni wapi kwenye PF3 tutaona wewe umemshona?

Shahidi: Maelezo yangu nilimshona.

Kibatala: Je, ulizungumza chochote kuhusu mahudhurio ya PC Fikiri kwenda kwa Mpasuaji?

Shahidi: Sikusema.

Kibatala: Kwanini ulitaka PC Fikiri aende kwa Mpasuaji?

Shahidi: Kesi ya maumivu ya kichwani kwake.

Kibatala: PC Fikiri aliruhusiwa lini?

Shahidi: Tarehe 18 Februari 2018.

Kibatala: Je ulimuuliza PC Fikiri kuhusiana na kufuata ushauri wako wa kwenda kwa mpasuaji?

Shahidi: Nilimuuliza.

Kibatala: Ulizungumzia kwenye ushahidi wako?

Shahidi: Sikuzungumzia.

Kibatala: Tungetegemea nini kama Fikiri angezingatia ushauri wako?

Shahidi: Tungekuwa na fomu ya vipimo.

Kibatala: Mtu anayekwenda kupiga X-ray anakuwa na nini kuthibitisha kuwa alipiga X-ray?

Shahidi: Film.

Kibatala: Uliona nyaraka yoyote ya kuthibitisha kuwa Fikiri alikuwa na amefanyiwa X-ray?

Shahidi: Sijaona.

Kibatala: Ni sahihi kuwa kuna faili la PC Fikiri pale Hospitali

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Umelitoa mahakamani?

Shahidi: Sikulitoa.

Kibatala: Nani anatakiwa kuzungumzia kuhusu hiko kitu kilichomjeruhi PC Fikiri?

Shahidi: Mimi.

Kibatala: Uliwahi kutoa amri juu ya PC Fikiri na Koplo Rahimu wasitembeleane hapo Hospitali?

Shahidi: Sikuwahi kutoa.

Kibatala: Kuna yeyote aliyekuwa ana magonjwa ya kuambukiza katika Koplo Rahimu na PC Fikiri?

Shahidi: Hakuna.

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote juu ya ndugu waliowatembelea PC Fikiri na Rahimu wakiwa pale Hospitali?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Kwa ufahamu wako uliwaona ndugu wa PC Fikiri na Koplo Rahimu?

Shahidi: Sikuwaoma.

Kibatala: Kwa ufahamu wako unafikiri kwanini PC Fikiri na Koplo Rahimu hawakupelekwa hospitali nyengine?

Shahidi: Sifahamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!