Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe, wenzake:Shahidi aibua mapya
Habari za SiasaSiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe, wenzake:Shahidi aibua mapya

Freeman Mbowe na viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea kusikiliza kesi namba 112 ya mwaka 2018 ya viongozi wa Chadema leo tarehe 1 Julai 2019.Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Shahidi wa tano wa Jamhuri, daktari aliyewatibu askari waliodaiwa kujeruhiwa kwenye maandamano yaliyofanywa na Chadema, ametoa ushahidi wake leo. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, shahidi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dk. Juma Khalfani ambaye ni Tabibu Msaidizi katika Hospitali ya Polisi ya Kilwa Road, ameeleza kuwa ingefaa zaidi kwa majeruhi wa maandamano kupelekwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo kulikuwa karibu zaidi na eneo la tukio.

Ametoa kauli hiyo akieleza kuwa, askari waliojeruhiwa Mkwajuni kwenye maandamano ya wafuasi wa Chadema walipelekwa mbali – Hospitali ya Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa.

Mashahidi wa awali walipoulizwa sababu za kupelekwa Hospitali ya Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa, hawakuwa wakieleza sababu.

Mashahidi hao hao walioulizwa kati ya Hospitali ya Mwananyamala nay a Kilwa, ipi nzuri zaidi, walidai ya Mwanayamala.

Pia walipoulizwa Hospitali ya Mwananyamala na ile ya Barabara ya Kilwa, ipo ipo mbali, walijibu hawawezi kukadiria umbali.

Hii ni tofauti kabisa na shahidi wa tano ambaye alidai, Mwananyama ilikuwa bora zaidi badala ya Hospitali ya Barabara ya Kilwa.

Jopo la Mawakili  wa Serikali liliongozwa na Faraja Nchimbi, Paul Kadushi, Wankyo Simon na Salimu Msemo huku upande wa utetezi, ukiongozwa na Profesa Abdallah Safari,  Peter Kibatala,  John Mallya na Hekima Mwasipu.

 Akimuongoza shahidi huyo wakili Msemo amemuuliza kuhusu majukuu yake alijibu kuwa, yeye ni daktari wa binadamu aliyeanza kazi zake mwaka 1991 na mwajiri wake ni Jeshi la Polisi.

Ameeleza licha kuwa, ni daktari ni Ofisa wa Jeshi hilo mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa jeshi hilo na kwamba mafunzo yake alihudhuria mwaka 1993.

Shahidi ameiambia mahakama kuwa, alianza kazi kwenye Zahanati ya Polisi iliyopo  Osterbay Polisi mwaka 1991 na baadaye kuhamia kwenye Zahanati ya FFU, Ukonga na Mwisho akawa daktari kwenye Hospitali ya Polisi ya Kilwa Road.

Alivyoulizwa kuhusu kumbukumbu zake siku ya tarehe 16 Februari mwaka 2018 ameeleza kuwa, siku hiyo alikuwa kwenye majukumu yake ya kazi.

Majira ya saa 5 usiku akiwa kwenye wodi ya wanawake wajawazito (wazazi), alifuatwa na muhudumu wa  kitengo cha dharura akamwambia kuwa,  wapo wagonjwa wawili wamekuja wakiwa wana hali mbaya.

Shahidi ameeleza kuwa, watu hao walikuwa ni PC Fikiri na Koplo Rahimu walijeruhiwa kutukana na maandamano ya liyofanyika eneo la Mkwajuni.

“Nilipoanza kumuliza PC Fikiri  aliniambia kwa mara ya mwisho alisikia kitu kizito kimemgonga shingoni, baada ya hapo hakujua kilichoendelea hadi anafikishwa hospitalini. Nikaamuru apelekwe wodini naye alipelekwa wodi ya wanaume,” amesema.

Shahidi ameeleza kuwa,  mgonjwa mwengine alimueleza kuwa yeye alipatwa na jeraha baada kupiga na kitu cha ncha kali.

Yafuatayo ni kipande cha mahojiano kati ya Shahidi na Wakili Profesa Safari.

Profesa Safari: Ulisema kuwa Rahimu na Fikiri walilazwa wodi tofauti?
Shahidi: Ndio
Profesa Safari: Kuna shahidi kati alisema walilazwa pamoja, sahidi hili limekaaje?
Shahidi: Kwa mujibu wake .
Profesa Safari: Unapajua Mkwajuni?
Shahidi: Napajua
Profesa Safari: Hospitali ya Mwananyala unaijua?
Shahidi: Naijua
Profesa Safari: Wapi mbali kwenu na Hospitali ya Mwananyamala?
Shahidi: Kwetu mbali
Profesa Safari: Kwa maoni yako kati ya kumpeleka Mwananyamala au Kilwa Hospitali?
Shahidi: Mwananyamala

Itaendelea mahojiano ya shahidi na mawakili wengine…

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!