Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Hatususi, haibiwi kura mtu
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Hatususi, haibiwi kura mtu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameapa wagombea wake kutoibiwa kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Pia amesema, chama chake hakitasusia uchaguzi huo na hakiko tayari kuona uchaguzi huo unavurugwa na vyombo vya dola ama mtu mmoja mmoja.

“Hatususi na hatutaliruhusu kuchakachuliwa” amesema Mbowe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uandikishaji wapiga kura nchini leo tarehe 15 Oktoba 2019.

Mbele ya wanahabari hao katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni, jijini Dar es Salaam Mbowe amesema, licha ya vikwanzo vya serikali ya Rais John Magufuli, uchaguzi huo watafanya vizuri.

Amewataka Watanzania kuacha kile alichokiita uaoga, na kwamba mabadiliko ya kiuchumi na kijamii hayatofikiwa ikiwa woga utatawala kwenye vifua vya Watanzania.

“…Hatuna sababu za kususia, sababu tutakuwa tunasusia maisha yetu na mustakabali wake katika kipindi cha miaka 5 ijayo,” amesema Mbowe.

Akizungumzia kusuasua uandikishaji wapiga kura unaoendelea kwa sasa, Mbowe amesema “haya ndio matunda ya siasa za Rais Magufuli.”

Amesema, Rais Magufuli anapaswa kuwa mtu wa kwanza kujilaumu, kutokana na aina ya siasa anayosimamia nchini katika kipindi cha miaka minne tangu aingie madarakani.

Kauli ya Mbowe inafuatia agizo la Rais Magufuli kutaka wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha, kwamba wananchi wanajiandikisha na baadaye wapige kura.

Hata hivyo, mwitikio wa wananchi katika uandikishaji huo umekuwa hafifu, kutokana na kukosekana msisimko wa watu kujitokeza.

“Rais atambue kwamba amezuia kazi ya siasa kwa miaka karibu minne, kujiandikisha na kupiga kura ni majumusiho ya michakato ya kisiasa iliyoendelea kwa miaka 4 iliyopita.

“Unazuia kazi ya siasa kwa miaka minne, halafu leo unawaambia Watanzania wajiandikishe wapige kura?” amehoji Mbowe.

Kwenye mkutano huo Mbowe amehoji, mgomo wa kujiandikisha umesababishwa na nani? Amesema “Wampigie kura nani ambaye ametufikia kwa miaka mine? Tupigie kura yupi ambaye tumempambanisha na mwenzake?

“Miaka minne CCM pekee ndio inafanya siasa katika nchi hii, kama wanachama wanaringa wanao, kwa nini wanachama wao hawaendi kupiga kura?”

Mbowe ameeleza kuwa, hatua ya Serikali ya Rais Magufuli kuvibana vyama vya siasa kufanya shughuli zake, imeshusha morali ya wananchi kujiandikisha katika zoezi hilo.

“Rais atambue kinachoendelea ni zao lake, na tutaendelea kuona kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020,” amesema Mbowe.

Mbowe ameishauri serikali kuruhusu vyama vya siasa, vifanye kazi ya kuhamasisha wananchi kwenda kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura, badala ya kutumia nguvu.

“Tunataka tumwambie Rais Magufuli, unaweza kumlazimisha ng’ombe au mnyama yoyote kwenda mtoni, lakini si kunywa maji.

“Acheni vyama vifanye kazi yake, vyama tunanyimwa hata kuhamasisha watu wetu kwenda kujiandikisha, mnategemea wapiga kura watatoka wapi wakati sisi wadau tunakatazwa?” amehoji Mbowe na kuongeza:

“Lakini wakuu wa wilaya, watendaji wa serikali na CCM wenye jukumu la kuhamasisha wananchi, uwezo huo hawana. Huko kukubalika kwa jamii CCM hawako, jamii ilishawahama muda mrefu wasiwalazimishe, wao walifikiri dola itasaidia kuwajenga wao kama chama.”

Mbowe amewataka viongozi wa Chadema kuhamasisha wafuasi wa chama hicho, na Watanzania kwa ujumla kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!