Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Haikuwa kazi nyepesi, tumeirudisha CCM kwenye reli
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Haikuwa kazi nyepesi, tumeirudisha CCM kwenye reli

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema haikuwa kazi nyepesi kufikia makubaliano ambayo yametangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba sasa mkwamo wa mchakato wa Katiba mpya utafufuliwa bila kuhodhiwa na chama chochote.

Amesema katika kipindi cha miezi saba ambayo ilikuwa ya ubishani mkubwa, wamefanikiwa kuirejesha CCM kwenye reli kwamba suala la Katiba ni la sasa na lazima lijadiliwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Januari, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais Samia dhidi ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

“Tumekuwa na ubishani wa muda mrefu, hatua ya kwanza ilikuwa kuwarejesha CCM kukubali kwamba suala la katiba sio la kusubiri ni suala la sasa, ilikuwa hatua muhimu sana kwetu kuwarudisha CCM kwenye hiyo reli kwamba suala la katiba ni suala la sasa na lazima lijadiliwe.

“Hatua ya pili ni namna ya kukwamua mchakato huo, tumekuwa na miezi saba haikuwa kazi nyepesi sana lakini hatimaye rais amekuja mwelekeo ambao tuliushauri sisi kwamba tuwe na mchakato ambao hautahodhiwa na chama cha siasa… kwamba uwe wote ikiwamo taasisi za dini yaani kiujumla uwe jumuishi.

“Hili jambo lilikuwa kikwazo sana cha mchakato huu kwa sababu huko nyuma ulikuwa umehodhiwa na CCM, nashukuru kupitia mazungumzo yetu ambayo sasa tunazungumza lugha inayoonekana kukubaliana kwamba huu mchakato usiwe unahodhiwa na chama chochote cha siasa ama kikundi chochote katika jamii. Uwe mchakato ambao unaleta Taifa pamoja namshukuru rais kwamba ameliona hilo,” alisema.

Amesema Taifa lilikuwa na uhitaji mkubwa wa demokrasia hivyo, tamko la Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu mikutano ya hadhara ni tamko chanya.

Aidha, amesema katika mazungumzo yake na Samia pamoja na viongozi wa chama chake na CCM yaliyofamnyika kwa nyakati mbalimbali, walizungumza mambo mengi ikiwamo yanahohusu haki za binadamu.

“Tulizungumzia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika nchi yetu, uchafuzi wa uchaguzi wa mwaka 2019 na uchaguzi wa 2020, ulazimu wa uwepo wa tume ya maridhiano na upatanishi katika Taifa kutibu wale ambao walipata madhila mbalimbali, yapo mengi lakini tuliyozungumza leo ni sehemu tu ya hayo na tutaendelea kuzungumza,” alisema na kuongeza kuwa.

“Chadema tunakuwa na misimamo kwa sababu tunakuwa na principal fulani zinazotuongoza, hatupingi wala hatubishi jambo kwa sababu tuna nia ya kupinga, tunapopinga au kubisha jambo ni kwa sababu tunaona haki fulani inakiukwa.

“Na wajibu wetu si kutetea haki ya chama chetu, vya vingine, watanzania wote, makundi yote na hatimaye Taifa letu,” amesema.

Amesema mchakato Katiba utaanza tena kwa sababu alichozungumza Rais Samia ni matokeo ya vikao kadha wa kadha walivyofanya.

“Ni mambo ambayo tumezungumza na tumekubaliana hivyo kwamba mchakato wa katiba lazima uanze. Hii ni sehemu ya mazungumzo yangu na yeye pamoja na vyama vyetu,” amesema.

Amesema jitihada zote hizo si kwa masilahi ya Chadema bali ni kwa masilahi ya vyama vyote na Tanzania kwa ujumla.

Kuhusu kurejea kwa viongozi wa Chadema kutoka ughaibuni ikiwamo Makamu wake, Tundu Lissu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema, Mbowe alisema kurejea kwao ni jambo la muda hasa ikizingatiwa kuimarika kwa utengamano katika taifa kunatia moyo.

Alisema muda muafaka ukifika viongozi hao watarejea nyumbani kwani hawakuenda huko kwa ajili ya uoga bali kuna mambo pia waliagizwa na chama kwenda kuyafanya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!