Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rungwe: Tumekula ubwabwa na kuanza mwaka kwa faraja tupu!
Habari za Siasa

Rungwe: Tumekula ubwabwa na kuanza mwaka kwa faraja tupu!

Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chaumma
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Taifa, Hashim Rungwe amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa kwao wapinzani ni faraja tupu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rungwe ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Januari, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais Samia dhidi ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Katika mkutano huo mbali na Rais Samia kutangaza kufuta zuio hilo la mikutano ya hadhara, pia ametangaza kuanza kwa mchakato wa marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwamo ya uchaguzi na vyama vya siasa pamoja na kuanza mchakato wa namna ya kuondoa mkwamo wa Katiba mpya.

Akizungumzia hatua hiyo, Rungwe amesema; “Tumeanza mwaka kwa tangazo zuri, sana, tumekuja kwa rais tumekula ubwabwa kwanza na kupata matangazo yake yaliyosheheni faraja kwamba tutakwenda kufanya mikutano ya hadhara bila vizuizi.

“Ni jambo la kufurahisha sana, tumeondoka zile zama za kutishana, nafikiri ni jambo jema, tunakwenda kwenye vitendo ili tuone kwani polisi wameelezwa vyake na sisi tumeelewa vyetu.

“Pongezi sana kwa rais na hii siku tulikuwa tunaisubiria sana. tuwe huru tuondokane na zile zama za kwamba … mimi nimeshasema!” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba mbali na kupongeza hatua hiyo, alisisitiza kuwa yale yanayohitaji kuundiwa kamati maalumu pamoja na marekebisho ya sheria, yasichukue muda mrefu hasa ikizingatiwa mwaka 2024 kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!