KIONGOZI wa ACT Wazalendo, Zitto kabwe amesema wamefarijika sana baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kufuta zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.
Ameongeza kuwa ni dhahiri kwamba Watanzania wameuanza mwaka vizuri hasa ikizingatiwa suala la mikutano ya hadhara ni jambo ambalo walikuwa wakilizungumzia siku nyingi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Zitto ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Januari, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais Samia dhidi ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.
“Leo rais kama alivyokuwa ameahidi siku zote, ametembea kwenye maneno yake. Kwa hiyo ni hatua kubwa kwetu sisi ni furaha, ndio maana mmeona alivyotamka hiyo tulisimama kushangilia.
“Lakini michakato ya marekebisho ya sheria mbalimbali kama ambavyo imependekezwa na vyombo mbalimbali pia kukwamuliwa kwa mchakato wa katiba ni mambo muhimu, naamini sote kwa pamoja tutaweza kufanya kazi vizuri na kuimarisha demokrasia na ya nchi yetu. Nakumbuka haikuwa hali ya kawaida lakini sasa hivi tumefanikiwa na tutakutana kwenye majukwaa ya kisiasa,” amesema Zitto.
Leave a comment