Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari Mawaziri kuzifuta machozi familia za wanahabari waliofariki ajalini
Habari

Mawaziri kuzifuta machozi familia za wanahabari waliofariki ajalini

Spread the love

 

MAWAZIRI wa Serikali ya Tanzania, wameahidi kutoa mchango wa fedha, kwa ajili ya kuzisaidia familia za wanahabari waliopoteza maisha ajalini, wakiwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 12 Januari 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloaji ya Habari, Nape Nnauye katika shughuli ya kuiaga miili ya wanahabari hiyo, iliyofanyika Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

“Mawaziri wenzangu wanatoa pole nyingi na wengi waliomba utaratibu wa kuchangia kidogo, kwa hiyo ule mchango wa Wanamwanza tutakuwa na mchango kwa ajili ya mawaziri katika kusaidia msiba huu, tuone namna ya kupunguza machungu ambayo wenzetu wamekutana nayo,” amesema Nape.

Wanahabari waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea jana tarehe 11 Januari 2022 mkoani Simiyu ni, Abel Ngapemba (aliyekuwa Afisa Habari Mkoa wa Mwanza) na Johari Shani (Uhuru Digital) ambaye pia alikuwa askari polisi.

Wengine ni, Husna Mlanzi (ITV), Steven Msengi (Afisa Habari Ukerewe) na Antony Chuwa (Habari Leo Online).

Nape amesema wanahabari hao ni mashujaa wa nchi kwa kuwa wamepoteza maisha wakiwa katika utekelezaji majukumu yao ya kazi.

“Nimekuja kuwasindikiza mashujaa ambao wamefia kazini, wamekufa wakitekeleza wajibu wao. Hawa kwenye tasnia ya habari ni mashujaa ndiyo maana mmewaona wanahabari wenzao pamoja na huzuni lakini wako hapa kuwasindikiza,” amesema Nape.

Awali, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, amesema uongozi wa Mkoa wa Mwanza, utatoa rambirambi zake kwa familia za wanahabari hao.

“Sisi kama mkoa tutayafanya yale ambayo Mungu ametupa neema kuyafanya kwa familia za wafiwa, ndiyo maana tumebeba msiba huu. Huu msiba ni wetu na tumeandaa rambirambi,” amesema Gabriel.

Baada ya miili hiyo kuagwa, mwili wa Husna Mlanzi utazikwa leo jijini Mwanza maeneo ya Kilimahewa na mili mingine imesafirishwa kwa ajili ya taratibu za mazishi nyumbani kwao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

Sekta ya Mawasiliano imekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi nchini-Mohamed

Spread the loveWaziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali Mapinduzi Zanzibar Khalid...

HabariHabari Mchanganyiko

TCRA yawataka wasafirishaji wa vipeto kujisajili na wengine kuhuisha leseni

Spread the loveMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa wito...

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

error: Content is protected !!