Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Matinyi: Uwekezaji bandari Dar neema kwa ICD
Habari Mchanganyiko

Matinyi: Uwekezaji bandari Dar neema kwa ICD

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi, amesema uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam unaenda kuchochea mafanikio kwenye Bandari Kavu (ICD). Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

DC Matinyi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kufanya ziara ya kukagua shehena inayohudumiwa na bandari kavu (Inland Container Depot – ICD) ya Harpended Explorer Scout Unit (HESU) iliyopo katika kata ya Miburani, wilayani Temeke.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mbunge wa jimbo la Temeke Dorothy Kilave, Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke  Nicodemas Tambo, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Temeke, George Sayi, pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Miburani, Abeid Mvuma.

Akizungumza katika ziara hiyo, mkuu huyo wa wilaya alisisitiza ushirikiano baina ya serikali na wawekezaji kwani uwekezaji unaotarajiwa kufanywa utaboresha zaidi bandari ya Dar es Salaam na kuiwezesha kuhudumia takribani tani milioni 38 za mizigo ifikapo mwaka 2030.

“Ubora wa huduma ya bandari hii umetokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kununua mitambo mitatu ya kupakua na kupakia makasha ya mizigo (Ship to Shore Gantry – SSG) ambapo mmoja una thamani ya shilingi bilioni 40 hadi 50.

Matinyi alieleza kuwa uwekezaji huu utasaidia kuhudumia nchi jirani kwa ukamilifu akizitaja Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Zambia, Malawi, Zimbabwe na hivi sasa hata Msumbiji, Komoro isiyokuwa na bandari kubwa na Sudan Kusini.

Amesema nchi hizo kwa mwaka zina shehena ya jumla ya zaidi ya tani milioni 70, hivyo sehemu ya shehena hii inahudumiwa na bandari za Mombasa, Beira, Maputo, Walvis Bay na Durban.

Kati ya tani milioni 21.27 ambazo bandari ya Dar es Salaam ilizihudumia mwaka 2022/23 ni tani milioni 8.5 tu ndizo zilizotoka katika nchi hizi.

“Mipango ya baadaye ya bandari ni kuboresha magati namba 8 hadi 11; kuhamisha kituo cha kupokelea mafuta na gesi kutoka Kurasini kwenda Kigamboni pamoja na kuongeza magati namba 12 hadi 15.

Awali serikali ilishatumia jumla ya dola za Marekani milioni 420 kujenga yadi namba 5 hadi 7 zenye uwezo wa kutunza makasha 10,000; kutanua na kuongeza kina cha mlango bahari wa kuingilia bandarini, kujenga gati namba 0 lenye urefu wa mita 320 na eneo la kutunza magari 6,000; kuongeza kina cha magati namba 1 hadi 7 kutoka mita 7 hadi 14.5 pamoja na upana wake kwa mita 15.

Matinyi  amefanya ziara hii ikiwa ni moja kati ya malengo yake ya kutembelea maeneo yote yanayojishughulisha na shughuli za kiuchumi wilayani Temeke.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!