Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matamko ya mali viongozi 46 yakutwa na dosari
Habari za Siasa

Matamko ya mali viongozi 46 yakutwa na dosari

Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama
Spread the love

 

KATI ya matamko 425 ya mali na madeni ya viongozi wa umma yaliohakikiwa, asilimia 11 (sawa na matamko 46) yalibainika kuwa na dosari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 21 Aprili 2022 katika hotuba ya makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka 2022/23 iliyowasilishwa na Waziri Jenista Mhagama.

“Uhakiki wa matamko ya rasilimali na madeni kwa Viongozi wa Umma na mgongano wa masilahi umefanyika kwa viongozi 425 kati yao, viongozi wanaume 302 na wanawake ni 123,” amesema Mhagama.

Amesema viongozi asilimia moja watafanyiwa uchunguzi wa kina na viongozi ambao tuhuma zitathibitika watafikishwa kwenye Baraza la Maadili.

Hata hivyo matamko 425 yaliyofanyiwa uhakiki ni sawa na asilimia 3 tu ya matamko 14,020 yaliyowasilishwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mhagama amesema matamko 14,020 yaliyopokewa ni asilimia 90.3 ya matarajio ya kupokea matamko 15,522 hadi kufikia Desemba, 2021.

Aidha amesema Malalamiko 115 ya ukiukwaji wa maadili dhidi ya Viongozi wa Umma yalipokelewa na kuchambuliwa.

“Kati ya malalamiko hayo, malalamiko 66 yalihusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na malalamiko 49 hayakuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hivyo yalipelekwa kwa taasisi husika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!