Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maswali sita Ngeleja kurudisha fedha za Rugemalira
Habari za SiasaTangulizi

Maswali sita Ngeleja kurudisha fedha za Rugemalira

Spread the love

KITENDO cha William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema kurudisha fedha alizopewa miaka mitatu iliyopita na mfanyabiashara James Rugemalira, kimezua maswali sita ambayo hayawezi kuwa na majibu, anaandika Hellen Sisya.

Ngeleja leo mapema alizungumza na waandishi wa habari na kueleza sababu zilizomfanya kurudisha fedha hizo alizorudisha kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuonesha risiti yake, huku akijinadi kuwa hakuwahi kuwa na kashfa katika kipindi chake cha uongozi.

Hapa chini ni taarifa iliyotolewa na Chadema kupitia kwa John Mrema, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

MAIGIZO YA NGELEJA HAYANA TIJA KWA TAIFA -NI ‘UTAKATISHAJI WA FEDHA’ HARAMU ZA ESCROW.

Leo Taifa limeshuhudia kituko kingine cha Karne baada ya Mbunge wA Sengerema, William Mganga Ngeleja kuitisha waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo ambao unamilikiwa na Serikali na kuamua ‘Kutakatisha’Fedha haramu za Escrow.

Nasema ametakatisha Fedha haramu kwani sote tumeshuhudia Rugemalila ambaye alimpa Ngeleja hizo Fedha Akiwa kizimbani na moja ya mashtaka aliyopewa ni pamoja na la ‘Kutakatisha ‘ Fedha .

Njia mojawapo aliyoitumia ‘Kutakatisha “hizo Fedha ni pamoja na kuwagawia watu mbalimbali akiwemo William Ngeleja ambaye naye amezirejesha Serikalini badala ya kuzirejesha kwa Rugemalila.

Ngeleja huyu Ametoa sababu ya kurejesha Fedha hizo ni ili kuepuka kashfa na anasema hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote . Anasahau kuwa ni juzi tu hapa ripoti ya Prof. Osoro maarufu kama ‘Makenikia’ ilimtaja tena kwa jina kuwa anahusika na ufisadi uliofanyika Katika sekta ya Madini Nchini alipokuwa waziri wa Nishati na Madini.

Ngeleja huyu alipokea Fedha hizo Mwaka 2014 na mwaka 2015 baada ya kelele kuwa Kubwa alilipa kodi TRA kiasi cha shilling 13 milioni, kutokana na kipato hicho.

Leo anajitokeza na kurejesha hizo fedha serikalini ambako baada ya kuzilipia kodi maana yake zilikuwa Mapato halali kwake na zilishatakata rasmi!

Ngeleja ameacha Maswali yafuatayo kwa kitendo chake hiki;

1. Je ? Kwanini amezirejesha serikalini badala ya kuzirejesha kwa Rugemalila (ambaye Ana kesi ya Kutakatisha Fedha zikiwamo na hizo alizokuwa amempa Ngeleja? )
2. Je ? Kitendo hiki sio cha kujaribu Kutakatisha hizo Fedha kwa kuzirejesha serikalini na hivyo kuharibu mwenendo wa kesi?
3.Kwanini Serikali imempa ukumbi wake ili akatolee hapo Tamko la kurejesha Fedha ambazo zina kesi ya Utakatishaji fedha Mahakamani?
4. Hivi kitendo cha Serikali kupokea fedha hizo hakuwezi kuathiri mwenendo wa kesi iliyoko Mahakamani? Kwani naamini kuwa wanufaika wa fedha haramu hizo ni sehemu muhimu ya kesi hii (kesi ya Escrow)
5.Tunaitaka Serikali iweke wazi fedha hizo zitaingizwa kwenye fungu lipi? Na Je kama Rugemalila ameshitakiwa kwa Kutakatisha fedha, hivi hati ya mashtaka itaenda kurekebishwa na hasa kwenye kiwango cha fedha kwani serikali imeshachukua sehemu ya fedha hizo kama Mapato yake halali .
6. Kitendo cha Ngeleja kurejesha fedha sio ushahidi tosha wa kumtia hatiani Ngeleja ? Anasalimika vipi huyu na Kesi iliyoko Mahakamani?

Mwisho ni kwanini Ngeleja amerejesha milioni 40.4 wakati alishalipia kodi ya zaidi ya milioni 13 kutoka kwenye fedha hizohizo? Nyongeza aliyoitoa serikalini ni kwa ajili ya kazi gani? Au ndio kukosa umakini?

Tunaamini kuwa serikali na Ngeleja watatoa majibu kwa umma juu ya igizo Hili la Ngeleja ambalo linaweza kabisa kuathiri mwenendo wa kesi iliyopo Mahakamani.

Imetolewa Leo tarehe 10 Julai ,2017.

John Mrema

Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!