May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manula ‘out’ dhidi ya Al Merreikh

Spread the love

 

KIPA namba moja wa klabu ya Simba, Aishi Manula anakosekana kwenye kikosi cha klabu hiyo kitakacho anza kwenye mchezo dhidi ya Al Merreikh. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Simba inashuka dimbani leo Jumamosi tarehe 6 Machi 2021, kwenye Uwanja wa Omdurman kuwakabili Al Merreikh kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika.

Kikosi kilichotolewa muda mfupi kabla kuanza mchezo huo saa 10:00 jioni, jina la mlinda mlango huyo tegemeo, halikuwepo kwa wachezaji wanaonza pamoja na akiba licha ya kusafiri na timu hiyo.

Pengine sababu kubwa ya mlinda mlango huyo kukosekana kwenye mchezo wa leo ni, kutokana kadhia aliyoipata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Kwenye mchezo huo, Manula aligongana na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Daniel Lyanga kwenye dakika ya 67 ya mchezo na kusababisha kupoteza fahamu na kupelekwa hospital.

Baada ya kupatiwa matibabu, Manula alirudi kikosi baada ya siku mbili na kujiandaa na safari ya kwenda sudan ambayo Simba waliondoka Jumatano tarehe 3 Machi 2021.

Kwenye mchezo huo na JKT Tanzania, Simba iliibuka na ushindi wa 3-0.

error: Content is protected !!