Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Katibu Mkuu mpya CCM huyu hapa
Habari za SiasaTangulizi

Katibu Mkuu mpya CCM huyu hapa

Paul Makonda
Spread the love

MJADALA wa nani atakayeshika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeanza kushika kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zinasema, wanachama kadhaa, wanatakwa kuteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kushika wadhifa huo.

Miongoni mwa wanaotajwa kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, ni pamoja na Paul Makonda, aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam; Dk. Kitila Mkumbo, waziri wa Uwekezaji na Nape Nnauye, mbunge wa Mtama.

Nafasi ya katibu mkuu wa CCM, imekuwa wazi baada ya Rais Magufuli, kumteuwa aliyekuwa akishirikilia nafasi hiyo, Dk. Bashiru Alli, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (CS).

Dk. Bashiru amekalia kiti cha Katibu Mkuu Kiongozi, baada ya kufariki dunia kwa Balozi John Kijazi, tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Benjamin Mpaka.

Mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online, ambaye ni mfanyakazi wa ofisi za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam na Dodoma anasema, “kuondoka kwa Dk. Bashiru kwenye nafasi hiyo, ni kama kulisubiliwa.”

Dk. Bashiru akizungumza kwa mara ya kwanza kmbele ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, mara baada ya kuteuliwa 29 Mei 2018

Anasema, wanachama walitamani ang’oke kwenye kiti hicho muda mrefu kwa madai kuwa ameshindwa kuvaa kiatu cha mtangulizi wake, Abdulrahaman Kinana.

Anasema, chini ya uongozi wake, chama kilikuwa kama hakipo na kimekuwa kikiendeshwa na mtu mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.

Dk. Bashiru ametumikia nafasi ya katibu mkuu kwa kipindi cha miaka miwili na miezi nane.

Alianza kutumikia nafasi ya katibu mkuu wa CCM, tarehe 29 Mei 2018, jina lake, kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, uliofanyikia Ikulu ya Dar es Salaam.

Tarehe 26 Februari 2021, Dk. Bashiru, aliteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.

Kada huyo amedai Dk. Bashiru na mwenezi wake, Hamphrey Polepole, walishindwa kabisa kukiimarisha chama hicho, na kwamba “bila mradi wa kununua wabunge na madiwani wa upinzani, CCM kingepotea kabisa.”

Lakini baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema, ni vigumu kumtabilia Rais John Magufuli, nani atamteua kushika nafasi hiyo.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Hii ni kutokana na hulka yake ya kuteua anayemtaka kwa kuamini anaweza kushika wadhifa fulani, bila kujali anatoka serikalini au ndani ya chama; na au nje kabisa ya CCM na mifumo yake.

Aidha, ugumu wa kubashiri nani anaweza kuwa mrithi wa Dk. Bashiru, unatokana pia na kanuni mpya aliyoianzisha Rais Magufuli ndani ya CCM ya mtu mmoja, cheo kimoja.

Hata hivyo, kuna wakati Rais Magufuli mwenyewe ameshindwa kusimamia kanuni hiyo; wapo watumishi wa CCM na Serikali, wenye vyeo zaidi ya kimoja.

Mfano halisi unaotajwa katika hilo, ni Polepole. Pamoja na kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais, lakini bado amebaki na wadhifa wake wa uenezi ndani ya CCM.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

Nape anatajwa kuwa huenda akafanywa kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala, kutokana na uzoefu wake wa uongozi ndani ya CCM na umri ufahamu wake wa baadhi ya mambo yanayoihusu CCM na serikali yake.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanampa nafasi ndogo mwanasiasa huyo kuteuliwa kushika nafasi hiyo, kutokana na kutojulikana msimamo wake halisi, katika baadhi ya masuala mazito ya nchi.

“Kuna wakati Nape anakuwa na msimamo mkali kwa baadhi mambo. Kuna wakati anaonekana kwenda kinyume na serikali na hata Rais Magufuli.

“Lakini kuna wakati anaweza kuunga mkono kila kinachotakiwa na watawala, kutegemeana yuko kwenye nafasi gani.”

Dk. John Magufuli

Naye Makonda, anabebwa na kukulia kwake ndani ya CCM na ushupavu wake wa kujibadilisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Moja ya vikwazo vinavyotajwa juu yake, ni azimio la serikali ya Marekani, lililomtaja kama mmoja wa watu waliozuiliwa kuingia nchini humo.

Mwanachama anayepewa nafasi kubwa ya kuwa chaguo la Rais Magufuli, kushika wadhifa wa katibu mkuu wa CCM, ni Prof. Mkumbo. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanampa Kitila nafasi kubwa kwa kuangalia utamaduni wa Rais magufuli wa kupenda kuwatumia watu waliotoka upinzani, kushika nyadhifa kubwa ndani ya CCM.

Prof. Kitila Mkumbo

Kama ilivyokuwa kwa Dk. Bashiru ambaye alitokea Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Mkumbo amepata kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) katika vyama vya ACT- Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Rais Magufuli aweza kumfanya Prof. Mkumbo katibu mkuu wa CCM na bado anaweza kumuacha kuendelea na wadhifa wake wa uwaziri.

Ni kama ambavyo Rais Benjamin Mkapa, alivyomteua Balozi Omar Ramadhani Mapuri kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na wakati huo huo, kuendelea kuwa Katibu wa Uenezi wa chama hicho.

Wengine waliowahi kushika nafasi mbili, ni pamoja na John Chiligati, ambaye alikuwa waziri wa Ardhi na Katibu mwenezi wa CCM; Yusuph Makamba, mbunge na katibu mkuu na George Mkuchika, Naibu Katibu Mkuu na waziri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!