May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgomo wa mabasi wanukia Tanzania

Mabasi yakiwa kituo cha mabasi Mbezi

Spread the love

 

CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), kimetoa siku tatu kwa mamlaka zinazohusika na mfumo wa mashine za kukatia tiketi kwa njia ya mtandao (POS), kutatua changamoto zinazoukabili “lasivyo hatuteweza tena kutoa huduma.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taboa wanalalamikia mfumo huo wakidai si rafiki na kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra), kuachana na mfumo huo kwani unawasababishia hasara.

Uamuzi huo, wameutoa leo Jumamosi tarehe 6 Machi 2021, katika kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

“Leo tarehe 6 Machi 2021, Taboa tumefanya mkutano mkuu wa dharura juu ya changamoto zinazotokana na mfumo huu ambao si rafiki wa POS, kumekuwa na faini za kila leo kutoka Latra bila kujali changamoto za mfumo.”

“Latra imekuwa ikifungia magari ya wamiliki wanaoshindwa kutumia mfumo bila kutatua changamoto za mfumo husika,” amesema mwakili wa wamiliki hao, Max Komba

“Hivyo basi, kwa kauli moja wanachama wameazimia kuwa, kwa kuwa mfumo wa kielekoniki si rafiki ni kandamizi, wasafirisgaji watashindwa kutoa huduma na tunatoa siku tatu kwa mamlaka kutatua changamoto,” amesema.

error: Content is protected !!