Saturday , 27 April 2024
Habari za Siasa

Mama Samia: Kazi ipo

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amewapongeza viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais John Magufuli, na kuwatahadharisha kwamba kazi ipo. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mama Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Oktoba 2019 wakati wa halfa ya kuwaapisha Wilson Charles, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kanali Wilbert Ibuge, Balozi na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mama Samia amewaambia viongozi hao kwamba, kama walivyoteuliwa usiku, na kazi zao watafanya hadi usiku, na kama walizoea kulala saa 4 usiku, basi wajiandae kulala kuanzia saa 9 Alfajiri.

“Kwanza hongereni, mi leo nilikua sina la kusema. Niwatakie kazi njema, kubwa ninaloweza kuwaambia kama mlikua mnalala saa 4 usiku, sasa hivi ni saa 9 alfajiri na pengine hata hiyo hamlali,” amesema Mama Samia na kuongeza;

“Sababu mi jana niko kama saa nane na dakika naona meseji, nikasema usiku huu hawa watu hawalali. Naangalia nikakuta hayo mambo, nikasema hongera zao walioteuliwa lakini kazi ipo . kama mlivyoteuliwa usiku na kazi hivyo hivyo karibuni kwenye uwanja huu tucheze kwa masilahi ya Watanzania.”

Rais Magufuli amewataka viongozi walioteuliwa kuivumilia kazi watakayokwenda kuifanya usiku na mchana.

“Na mimi nawapongeza kachapeni kazi, kamtangulizeni Mungu katika kazi zenu. Kama alivyosema Mheshimiwa makamu wa rais  na mawaziri,  kazi hizi ni za usiku na mchana kwa hiyo mkavumilie. Kazi hizi ni za utume kwa hiyo mkawatumikie watanzania,” amesema Rais Magufuli.

Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amemkaribisha Charles katika ofisi yake mpya na kumjuza kwamba kuna majukumu mengi yanayomsubiri mezani kwake.

Aidha, Jaji Kaijage amemkabidhi zoezi la uandikishaji majina ya wapiga kura linaloendelea nchini.

“Kwa upande wa Dk. Charles mimi kama mwnyekiti nakukaribisha sana.  Kwa ufupi tume inaendeshwa kwa katiba na sheria za uchaguzi kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais na madiwani zoezi hilo hivi sasa kama unavyojua linaendelea Tanzania nzima,” amesema Jaji Kaijage na kuongeza.

“ Na kwa hivi sasa ninavyozungumza, meza yako ina shughuli nyingi sana. Nadhani ukitoka hapa ukazikabili, lakini siku ya leo si mambo mengi ni kukupongeza karibu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!