Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makontena ya Makonda kupigwa mnada J’mosi
Habari za Siasa

Makontena ya Makonda kupigwa mnada J’mosi

Spread the love

BAADA ya mnada wa kwanza wa makontena 20 yenye samani yaliyoingizwa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukwama, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imepanga kufanya mnada wa pili Jumamosi ya Septemba mosi, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

TRA imetaarifu kuwa, imedhamiri kurudia mnada huo wa makontena yenye samani za ofisi ikiwemo meza na viti, ambayo yamekwama katika bandari kavu ya Dar es Salaam kutokana na kudaiwa kodi ya kaisi cha Sh. 1.2 bilioni.

Mamlaka hiyo imetoa wito kwa wananchi kujitokeza katika mnada huo kununua samani hizo kwa kufuata taratibu na sheria za minada.

Aidha, TRA imewatoa hofu wananchi kuhusu kauli iliyotolewa na Makonda ya kwamba atakaye nunua makontena hayo atalaaniwa na Mungu.

Baada ya mnada wa kwanza uliofanyika tarehe 25 Agosti, 2018 kukwama kutokana na wateja kushindwa kufika bei elekezi, Makonda alitoa kauli akisema kuwa, mtu atakayenunua makontena hayo atapata laana kwa kuwa, makontena hayo yenye samani yaliingizwa nchini kwa ajili ya kuwasaidia waalimu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!