Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kundi la paka lashiriki mazishi
Habari Mchanganyiko

Kundi la paka lashiriki mazishi

Spread the love

KUNDI la paka wapatao 12 wameshiriki mazishi ya Salehe Matiko aliyezikwa saa 10 alasiri ya Agosti 24 katika Kijiji cha Chikalala mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Maalumu … (endelea).

Matiko aliuawa kwa kushambuliwa na wakazi wa kijiji hicho kwa tuhuma za ushirikina huku akidaiwa kuwatesa watu ikiwa ni pamoja na kuua ndugu zake.

Wananchi wa kijiji hicho walieleza kuchoshwa na kile walichokiita mateso ya Matiko na kuamua kumwinda na kumshambulia mpaka kupoteza maisha yake.

Wakiwa msibani baada ya taratibu zote za kuandaa safari ya Matiko, jeneza lake lilibebwa kwa utaratibu wa kawaida lakini ghafla wakiwa barabarani kuelekea makaburini liliibuka kundi la paka lililokuwa lifuata jeneza hilo kwa nyuma.

Hali hiyo iliibua hofu lakini wanakijiji hao walipiga moyo konde na kuendelea na safari ya makaburini ambapo paka hao nao walifika kwenye eneo hilo wakiwa katika kundi lao.

Wakati wa kushusha maiti kwenye kaburi lake, paka hao waliinamisha vichwa chini wakionesha utii wao kwa marehemu jambo ambalo liliwashtua wengi.

Baada ya kumaliza taratibu zote za kumuhifadhi Matiko watu walioshiriki mazishi hao walitawanyika kama ilivyo ada lakini paka hao hawakutawanyika na badala yake waliendelea kubaki makaburini hapo.

Msafiri Msemwa ambaye ni mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa, waliingia hofu kidogo kwa kuwa sio tukio la kawaida lakini waliendelea na taratibu za mazishi hayo.

“Sio jambo la kawaida kutokea ndio maana kila mmoja alikuwa na hofu lakini watu waliendelea kama kawaida mpaka mwisho.

“Kila mmoja alikuwa na tafsiri yake kutokana na kundi hilo la paka ambapo muda wote wa mazishi watu walikuwa wakiwatolea macho paka hao huku wakichukua tahadhari kwa lolote ambalo lingeweza kutokea,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!