July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makinda: Ni aibu kutohesabiwa

Anna Makinda, Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara

Spread the love

 

KAMISAA wa Sensa upande wa Tanzania Bara, Anne Makinda amewataka Watanzania wajione fahari kuhesabiwa kwa kuwa ni aibu kutohesabiwa katika sensa ya mwaka 2022. Anaripoti Glory Masamu TUDARCo … (endelea).

Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Septemba katika uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 jijini Dodoma.

Amesema sensa ya sasa itakuwa shirikishi na itaanzia ngazi ya vitongoji hivyo viongozi wa vitongoji vyote lazima watambue umuhimu wa zoezi hilo.

Ametoa wito kwamba siku ya kuhesabiwa itakapofika kila mtu akimbilie kuhesabiwa.

“Sensa itatufanya tujulikane tuko wangapi…kweli mwenyekiti wa kitongoji utashindwa kuwajua watu wako?

“Vitongoji wote tukihesabu watanzania wote watakuwa wamehesabiwa, mtanzania mwenzangu jitokeze uone fahari kuhesabiwa, ukiwa hukuhesabiwa usimwambie maana ni aibu,” amesema.

error: Content is protected !!