Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamba amwakilisha Samia mkutano wakuu wa nchi Italia
Habari za Siasa

Makamba amwakilisha Samia mkutano wakuu wa nchi Italia

Spread the love

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewasili Roma, Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 – 29 Januari 2024, Roma, Italia.

Mara baada ya kuwasili, Makamba amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mohmoud Thabit Kombo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo wa wangazi ya Wakuu wa Nchi wa Afrika na Italia, unatarajiwa kujadili ajenda mbalimbali zikijumuisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu, ushirikishwaji wa wahamiaji katika kuleta maendeleo, usalama wa chakula, mapambano dhidi ya ugaidi na matumizi ya teknolojia ya kidigitali.

Ajenda nyingine ni pamoja na uhamiaji haramu, mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, mabadiliko ya tabianchi, ushirikiano katika sekta ya elimu kupitia ngazi ya vyuo vikuu na katika mafunzo ya ufundi na utamaduni.

Kupitia mkutano huo Serikali ya Italia inatarajia kujipambanua kama mshirika muhimu wa maendeleo wa bara la Afrika kupitia mpango mpya wa maendeleo utakaotambulishwa kwa mara ya kwanza uitwao Mattei Plan.

Mpango huo unalenga kuifanya Italia kushirikiana kwa karibu na bara la Afrika katika nyanja za maendeleo ya usawa na unatarajiwa kutambulishwa kwa nchi zingine za Umoja wa Ulaya hapo baadae utakapoanza utekelezaji.

Vilevile kupitia Mkutano huo Italia inatarajia kutangaza kuunga mkono umuhimu wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) kuwa mwanachama kwenye Kundi la G-20.

Kadhalika, Italia inatarajia kutumia fursa ya mkutano huo, kuonesha utayari wake wa kuhamisha teknolojia ya kisasa (the know-how) katika sekta ya kilimo kwa nchi za Afrika na kuwa kitovu cha usambazaji wa Nishati kutoka Bara la Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!