Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yajifungia kuchagua watendaji wa mikoa, majimbo
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yajifungia kuchagua watendaji wa mikoa, majimbo

Spread the love

IKIWA umesalia takribani mwezi mmoja kwa Chama cha ACT-Wazalendo kufanya uchaguzi wake mkuu, chama hicho kimefanya kikao cha kuteua makatibu wa mikoa na majimbo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma ACT-Wazalendo, Janeth Rithe uteuzi huo utafanyika katika kikao cha Kamati Kuu kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho unaoatarajiwa kufanyika Machi mwaka huu.

Katika hatua nyingine, taarifa ya Rithe imesema kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa nchini.

“Chama chaACTwazalendo kitafanya  kikao cha Kamati Kuu kujadili masuala mbalimbali ya ndani ya chama na taifa kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine kikao hicho kitateua makatibu wa majimbo na mikoa Tanzania Bara na Zanzibar,”

“ Itapitia Taarifa ya Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama, Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Taifa utakaochagua viongozi wa chama ngazi ya Taifa utakaofanyika mwezi Machi, 2024, Hali ya Kisiasa nchini,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!