Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Oryx Gas yakabidhi mitungi 700 kwa waziri Jafo
Habari Mchanganyiko

Oryx Gas yakabidhi mitungi 700 kwa waziri Jafo

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk. Selemani Jafo wamekabidhi  mitungi 700 ya gesi pamoja na majiko yake kwa walimu 500 pamoja na Baba na Mama Lishe 200 yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 50 katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

Pia  huku imeahidi kufunga mfumo wa gesi katika Shule ya Sekondari Minaki ili waanze kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi hiyo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Wilaya ya Kisarawe Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema anamshukuru Waziri Jafo, kwa kumpatia nafasi ya kupeleka nishati safi ya kupikia kwa walimu pamoja na Baba na Mama lishe wilayani Kisarawe.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Salemani Jafo wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 700 yakiwa na na majiko yake kwa walimu pamoja na baba na mama lishe katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani

“Oryx Gas tunaamini kwamba ukipika kwa kutumia gesi, inaleta maendeleo mengi kwa jamii yetu. Kupika kwa gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti. Zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.

“Wanawake wanatumia muda mchache kupika hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula, na wanaume pia watajiongezea marks ukiwazadia wamama mitungi ya gesi.Kwa kutumia gesi ya Oryx, Watoto wanakua na muda mwingi zaidi kusoma na sio kwenda kutafuta kuni,” anasema.

Amesisitiza kuwa kuanzia Julai mwaka 2021 wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali waliyopokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Araman amesema kupitia mipango hiyo  Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa  ambayo si tu mbaya kwa afya bali pia ni hatari kwa mazingira yetu  huku akitumia nafasi hiyo kueleza pia Oryx Gas inatekeleza juhudi za kueneza matumizi ya nishati safi kwa Watanzania wengi ipasavyo ambayo ni ndoto kubwa ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan.


Pia amesema Oryx Gas inatekeleza agizo la Serikali kwa kuhakikisha taasisi zenye watu zaidi ya 100  kutumia nishati safi kwa kutengeza mifumo salama ya gesi kwa kutumia tenki kubwa ambapo mifumo hiyo inaweza tumika shuleni, kambi za jeshi, vyuo vya polisi, magereza na katika kampuni za uzalishaji.

“ Hii inasaidia kupunguza matumizi ya mafuta machafu kwenye mifumo ya uzalishaji. Oryx Gas Tanzania inajipongeza kwa kujulikana kua kampuni kinara katika usambazaji wa gesi ya kupikia majumbani kwa Watanzania kwa sasa. Sisi Oryx Gas Tanzania tutaendelea kuwekeza zaidi katika kuratibu kubadilisha na kueneza nishati safi kutumika na Watanzania kwa kutumia gesi ya Oryx kwa manufaa yetu wote.”

Pia amehimiza wananchi kutumia gesi ya LPG katika shughuli zao  mbalimbali ili kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzania na kwa ajili ya kuboresha Maisha yetu kiujumla huku akitumia nafasi hiyo kueleza Waziri Jafo amekuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa waalimu na jamii kiujumla kwa kuunga mkono katika  mpango huo wa matumizi ya nishati safi wilayani Kisarawe.

Akizungumzia kuhusu kufunga mfumo wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya sekondari ya Minaki , Aramn amesema watafunga mfumo huo ili shule hiyo kuondokana na kutumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia na kwamba Orxy itafunga mfumo wenye uwezo wa kubeba ujazo wa tani moja ya gesi na ametoa ahadi hiyo baada ya Waziri Jafo kutoa ombi kwa kampuni hiyo kufunga mfumo huo katika shule hiyo ambayo yeye amesoma kidato cha tano na sita.

Kwa upande wake Waziri Jafo ametumia nafasi hiyo kuishukuru Oryx kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa vitendo huku akieleza kuwa tayari Serikali imeshatoa maelekezo kuanzia mwaka huu wa 2023  taasisi , mashirka na maeneo ambayo yana watu kuanzia 100 kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo nishati ya gesi.

Akizungumzia zaidi Waziri  Jafo amesema mbali ya kugawa mitungi ya gesi kwa walimu 500 bado ataendelea kuzungumza na wadau ili apate mitungi mingine kwani lengo lake ni kuhakikisha walimu wote 1300 walioko katika wilaya hiyo wawe wamepata mitungi ya gesi.

“Idadi ya walimu waliko Kisarawe ni 1300 hivyo baada ya kugawa majiko 500 yatahitajika tena majiko 800 ya gesi lakini hili suala tutaendelea kuwafikia wadau .lengo langu kila mwalimu wa Kisarawe awe na gesi. Pia nimemuomba Mkurugenzi wa Oryx atufungie mfumo wa gesi katika sekondari yetu ya Minaki na amekubali na huu ni mwanzo tu kwani nataka kuona shule zote za Kisarawe tunafunga mfumo huo ili kuondakana na matumizi ya kuni na mkaa,”amesema Waziri Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!