Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Majaliwa azungumzia hali ya corona Tanzania
AfyaHabari za Siasa

Majaliwa azungumzia hali ya corona Tanzania

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa COVID-19 ambao umeanza kupungua nchini humo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumapili, tarehe 24 Mei, 2020 wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Fitri katika Msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma

Taarifa iliyotumwa kwa umma na ofisi ya waziri mkuu, imemnukuu Majaliwa akisema, wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Kiongozi huyo, amewasisitiza wasiwe na hofu na waendelee kufanya kazi kwa bidii.

Kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID-19 ilivyo kwa sasa nchini, Majaliwa amesema, katika hospitali ya Amana yupo mgonjwa mmoja, Mloganzila yupo mmoja, Temeke hatuna mgonjwa aliyethibitishwa na Kairuki hakuna mgonjwa.

Pia, amesema, Rabiansia hakuna mgonjwa, Regency hakuna mgonjwa, Aga Khan yuko mgonjwa mmoja, Lulanzi Kibaha wapo wagonjwa 16 na Dodoma Mkonze mpaka leo asubuhi wapo wagonjwa tatu.

Katika hotuba yake, Majaliwa amesema, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewapongeza Waislamu wote nchini kwa kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na anawashukuru kwa namna walivyoshiriki kuliombea Taifa hasa  katika kipindi hiki cha kukabilia na ugonjwa wa corona.

Pia, Rais Magufuli amewashukuru waumini wa dini nyingine nchini kwa kushiriki kikamilifu kwenye kuliombea Taifa.

“Leo hii tunamalizia dua ya kumshukru Mwenyezi Mungu, jambo hili Mheshimiwa Rais anasema hatasahau kwa viongozi wote wa dini kuwa pamoja kuliombea Taifa,” amesema Majaliwa

“Pia, Mheshimiwa Rais amesema tuendelee na dua zetu, kila mmoja kwa imani yake wakati wote ili Mwenyezi Mungu aendelee kutuondoa katika janga hili ambalo limeleta mtikisiko duniani kote,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania wote kwa ujumla waendelee kushirikiana katika kulifanya Taifa liwe la amani na utulivu.

“Dini zetu zinatutaka kila mmoja aendelee kuomba, nchi hii imekuwa na utulivu sana na mfano duniani kwa nchi zinazotaka amani,” amesema

“Tuendelee na tabia hii na viongozi wa dini endeleeni kusisitiza suala la amani, Serikali inawasisitiza muendelee na shughuli zenu, sisi tutahakikisha tunaendelea kulinda amani, fanyeni kazi, mkulima lima na kwa walio viwandani nao waendelee kufanya kazi,” amesema

Awali, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab, amempongeza Rais Magufuli kwa kuwapa Watanzania moyo wa kishujaa na ujasiri katika kukailiana na ugonjwa wa COVID-19 kwa kuwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili aliepushe Taifa na janga hilo, wakati Mataifa na viongozi wengine duniani yakikumbwa na taharuki.

“Hakuna mkombozi zaidi ya Mwenyezi Mungu, shida zetu, matatizo yetu na hata tukijaribiwa kwa maradhi au mtihani wa aina yoyote  Mwenyezi Mungu anatupa ushujaa wa kukabiliana nao. Hofu ya maradhi ni kifo hivyo tusiwe na hofu tumtegemee Mwenyezi Mungu kama Rais wetu anavyotusisitiza,” amesema.

Amesema wananchi hawana sababu ya kuwa na hofu kwani tayari Rais Magufuli alitangaza siku tatu kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu aliepushe Taifa na corona na viongozi wa dini zote  waliitikia wito na waliongoza maombi ambayo yamejibiwa na sasa huo ugonjwa umepungua nchini.

Sheikh Rajab aliongeza baada ya Mwenyezi Mungu kukubali dua hizo na Rais Magufuli, kutenga siku tatu za kumshukuru Mwenyezi Mungu ambazo zinaisha leo, wananchi hawana budi waendelee kumshukuru na kamwe wasishiriki kwenye kufanya maasi.

“Tuwe ni watu wenye kushukuru neema tunazojaaliwa na Mwenyezi Mungu na kamwe tusiwe wenye kuzikufuru,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!