Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa atoa maagizo kwa wenyeviti vijiji, vitongoji
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atoa maagizo kwa wenyeviti vijiji, vitongoji

Spread the love

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji kutekeleza majukumu yao kwa uwazi, ikiwemo kuitisha mikutano ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi…(endelea).

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, tarehe 14 Aprili 2022, akifungua mafunzo ya utawala bora ya viongozi ngazi ya kata na vijiji, wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi.

“Niemsikia kuwa ipo mada ya utawala bora na hasa uwazi na uwajibikaji. Jambo hili ni muhimu sana, wewe kama kiongozi kila unachokifanya hakikisha kinakuwa wazi. Hakuna haja ya kuficha, hili jambo lina maslahi kwa umma kwa hiyo suala la uwazi na uwajibikaji ni muhimu sana,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amewaagiza viongozi hao wa vijiji, kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali, ikiwemo ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Nendeni mkawe wawazi, uwazi ni moja ya msingi mkubwa wa utawala bora, niwatake viongozi wote kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kila siku za shughuli za kijiji chenu. Nendeni mkaitishe vikao vya vijiji,” amesema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo amewataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji, wakahamasishe mbio za mwenge zinazoendelea nchini.

“Nendeni mkahamasishe mbio za mwenge kama moja ya alama za nchi yetu, mwenge ni alama ya taifa, falsafa yake kuwaunganisha Watanzania kuwa pamoja. Mwenge una kazi kubwa kuhamasisha maendeleo kwenye nchi hii na lengo nchi iwe kwenye maendeleo tupae ikiwezekana tuzidi nchi zote,” amesema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Majaliwa amewataka waheshimu mipaka ya madaraka yao.

“Inawezekana mmekuja hapa wenyeviti wa vijiji na vitongoji, wote ni wenyeviti lakini mtambue mipaka yenu, isije tukasikia kuna migogoro ya mwenyekiti wa kijiji.

“Hakuna sababu ya kugombana na kama mamlaka zinafanana mnagombania juu ya jambo linalohusisha pande mbili, hakuna haja ya kutunishia misuli, tuna sheria na kanuni lazima zizingatiwe,” amesema Waziri Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!