Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Mtunisha misuli nyota wa Marekani afariki dunia
Burudika

Mtunisha misuli nyota wa Marekani afariki dunia

Spread the love

MJENGA misuli wa Marekani Cedric McMillan amefariki akiwa na umri wa miaka 44, baada ya miaka kadhaa ya matatizo ya kiafya yaliyosababishwa na Covid-19, na ajali ya barabarani. Anaripoti Rhoda Kanuti …(endelea).

McMillan, mkongwe wa muda mrefu wa Jeshi la Marekani na Walinzi wa Kitaifa, alikuwa mjenga misuli mkongwe na mshindi wa 2017 wa taji la kifahari la Arnold Classic.

Kwa mujibu wa taarifa ya kifo chake kimedhibitishwa leo tarehe14 Aprili 2022 na mfadhili wake Black Skull USA katika mtandao wa Instagram.

Amesema “tunasikitika kuwafahamisha kuwa rafiki, kaka yetu @ cedricmcMillan amefariki leo’’

Black Skull USA amesema kwenye Instagram kwamba Cedric atakumbukwa kama mwanariadha, mwanachama mwenzao rafiki na baba.

Hata hivyo, ni kifo cha tatu kwa mjenga misuli mashuhuri nchini Marekani, kufariki tangu mwaka uliopita.

McMillan amefariki akiwa na umri wa miaka 44, amekuwa mtaalam wa kujenga misuli tangu mwaka 2009, kabla ya kushinda mfululizo mashindano katika kilele Arnod Classic mwaka 2017.

Mashindano hayo huandaliwa na taasisi hiyo ya mjenzi wa misuli, mwigizaji na gavana wa zamani wa Califonia, Arnod Schwarzenegger.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!