May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango ataka kamati usuluhishi migogoro viongozi wa dini

Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais, Dk. Phillip Mpango, ameshauri kamati za amani ziundwe kwa ajili ya kutatua migogoro inayoibuka katika nyumba za ibada. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Mpango ametoa wito huo jana Jumatano, tarehe 13 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam, katika futari iliyoandaliwana na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Natamani sana kila dhehebu tuwe na kamati ya amani ya viongozi wa dini, lakini natamani kila dhehebu liwe na kamati ya amani ambayo itafanya kazi usiku na mchana kulea na kutafuta amani ndani ya madehebu yetu mbalimbali ya dini,” amesema Dk. Mpango.

Dk. Mpango amesema, Serikali inaumizwa na migogoro ya ndani ya makanisa na misikiti.

“Viongozi wangu wa dini mtafute kwa bidii na kuomba amani itawale katika nyumba za ibada, Serikali na bila shaka wengi wenu tunakerwa na kuumizwa sana na mighogoro ndani ya makanisa na misiti, ikiwemo kugombea uongozi na matumizi mabaya ya madaraka na mali za kanisa au msikiti,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Mambo ambayo yanakwenda kinyume na katiba za madhebu husika na hata maandikio matakatifu.”

error: Content is protected !!