Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Majaliwa aeleza siri yake na Kikwete “kanitoa darasani”
Tangulizi

Majaliwa aeleza siri yake na Kikwete “kanitoa darasani”

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, ana mchango mkubwa katika safari ya maisha yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Majaliwa amebainisha hayo leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021, wakati akizindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26, jijini Dodoma.

Viongozi mbalimbali wa serikali na kisiasa wamehudhulia hafla hiyo akiwemo, Kikwete aliyeongoza taifa hilo kwa nafasi ya urais kwa miaka kumi kuanzia 2005 hadi 2015.

Majaliwa mwenye miaka 59 amesema, Kikwete ndiye aliyemtoa katika kazi ya ualimu mwaka 2005, baada ya kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.

Amesema, nafasi hiyo alihudumu kwa muda wa miaka mitano, hadi 2010 alipoamua kuingia kwenye siasa na kwenda kugombea Ubunge wa Ruangwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Lindi.

“Katika hili na mimi nitumie nafasi hii kumshukuru Kikwete, ndiyo alinianzishia kufanya kazi ya utumishi ndani ya Serikali.”

“Kikwete alinitoa darasani na kunipa ukuu wa wilaya kwa mara ya kwanza 2005. Na nilipohudumu kwa miaka mitano nafasi ya ukuu wa wilaya, nikajikimbiza jimboni kupata ubunge,” amesema Majaliwa aliyezaliwa tarehe 22 Desemba 1961.

Mbunge huyo wa Ruangwa, amesema baada ya kupata ubunge 2010, Kikwete alimteua tena kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, anayeshughulikia elimu, nafasi aliyohudumu kwa muda wa miaka mitano (2010-2015).

“Nilipopata ubunge, akaniteua tena kuwa naibu waziri wa elimu, kwa nafasi ambayo nilihudumu pia miaka mitano. Hivyo uwepo wa mimi hapa jukwani na uwepo wake kwangu, lazima niringie kwa sababu ana mchango mkubwa sana katika maendeleo yangu,” amesema Majaliwa.

Mwaka 2015, Majaliwa aligombea tena jimbo hilo na kufanikiwa kushinda, kisha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli, alimteua kuwa waziri mkuu, nafasi anayohudumu mpaka sasa.

Hayati Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, na mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi 2021.

Aliiongoza Tanzania kwa muda wa miaka mitano na miezi mitano mfululizo kuanzia 5 Novemba 2015 hadi 17 Machi 2021.

Baada ya Rais Samia kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kifo cha Hayati Magufuli ambapo alifanya mabadiliko ya baraza la mawaziri, Majaliwa ameendelea kusailia kwenye nafasi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!