May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jacob Zuma afungwa jela miezi 15

Jocob Zuma, Rais mstaafu wa Afrika Kusini

Spread the love

 

MAHAKAMA nchini Afrika Kusini, leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021, imemhukumu kifungo cha miezi 15 gerezani aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jacob Zuma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hii ni baada ya mahakama ya Katiba kumtia hatiani kwa kukaidi agizo la kufika mahakamani baada yakukosa kufika kwenye kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.

Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama, Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo, aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.

Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.

Wafanyabiashara walishutumiwa kwa kula njama na wanasiasa kushawishi mchakato wa kufanya maamuzi ya serikali Rais huyo wa zamani alijitokeza mara moja kwenye uchunguzi wa kile kilichojulikana kama “kukamatwa kwa serikali” lakini akakataa kujitokeza baadaye.

Uchunguzi huo – ulioongozwa na Jaji Raymond Zondo – uliuliza mahakama ya Katiba iingilie kati. Haijulikani ikiwa Zuma sasa atakamatwa.

Katika suala tofauti la kisheria, Zuma alikataa hatia mwezi uliopita katika kesi yake ya ufisadi iliyohusisha makubaliano ya silaha ya dola bilioni 5 kutoka miaka ya 1990.

error: Content is protected !!